D’Jaro Arungu

mtangazaji maarufu kutoka nchini Tanzania

D'Jaro Deus Arungu (20 Februari, 1979 - Rorya, Mara) ni mtangazaji maarufu kutoka nchini Tanzania. Hujulikana zaidi kwa jina la Baba Mzazi na pia kwa kuwa mtangazaji mkuu wa kipindi cha Papaso kupitia TBC FM (zamani PRT)[1][2] kinachorushwa kuanzia saa moja usiku hadi saa nne usiku. Ambapo amekuwa katika kipindi hicho tangu kuanza kwake mnamo 2015 hadi sasa.

D’Jaro Arungu
Agosti 7, 2022 - katika studio za TBC FM.
AmezaliwaD'Jaro Deus Arungu
(1979-02-20)20 Februari 1979
Majina mengine
  • Baba Mzazi
  • Mzee wa Papaso
Asili yakeMara, Tanzania
Kazi yake
  • Mtangazaji
  • mwanahabari
  • mwandishi wa habari
DiniMkristo

Maisha ya awali

Usuli wake

D'Jaro Deus Arungu alizaliwa katika Mkoa wa Mara, wilaya ya Rorya mnamo tarehe 20 Februari, 1979. Alisoma shule mbalimbali za msingi tangu 1989 hadi 1995. Kuanzia Shule ya Msingi Manyara, Shule ya Msingi Omoche A, Shule ya Msingi Masike.

Baadaye shule ya sekondari Vosa Missionary halafu elimu ya juu Benjamini Willia Mkapa. Akajapa kupata stashahada katika chuo cha uandishi wa habari cha 'The Royal College kati ya 2006-2010. Ambapo alihitihamu na Stashada ya Juu katika uga wa uandishi wa habari.

Akaja kuchukua Bachelor of Arts in Mass-Communication katika Chuo Kikuu Tumaini (Tumaini University Dar es Salaam College - TUDARCO) - 2015-2018.

Kazi

Alianza kazi ya kupiga picha mbalimbali baada ya kumaliza sekondari. Katika upigaji huu wa picha ndipo alipoangukia utangazaji.

Utangazaji

D'Jaro alikuwa na ndoto za kuwa mtangazaji miaka mingi tangu enzi za ujana wake. Imekuwa sadfa kwake kujikuta katika mikono ya utangazaji mapema mnamo mwaka 2001. Huo ulikuwa mwaka aliojiunga Times FM na kazi yake ilikuwa kutoa ripoti ya vipindi vya michezo pekee. Times alitoka 2002 akajiunga Kiss FM hadi 2003. Ilipotimu 2004, akajiunga PRT Radio (sasa hivi TBC FM) ambapo yupo hadi sasa. Hapa aliingia kama mtangazaji wa kipindi cha Salamu. Kipindi ambacho kilikuwa kinaanza saa 11 jioni hadi saa 12. Zaidi ilikuwa salamu na muziki. Akaja kutokea katika vipindi vingi moja wapo ikawa Ladha za Afrika Mashariki (2006 - 2008 - Top Ten - hakipo tena), Swaga za Kikwetu (2008), Bunga Bonga na hatimaye Papaso tangu 2015.[3]

Tuzo alizoshinda

Zifuatazo ni baadhi ya tuzo alizoshinda.

  1. Tuzo za Watu - Mtangazaji na Kipindi Bora PAPASO (2015)[4][5][6]
  2. Tanzania Instagram Awards (2016) Mtangazaji Bora wa Vipindi vya Radio

Marejeo

  1. Mtanzania Digital (2017-05-20). "D'JARO ARUNGU ASIMULIA MSOTO, MPETO". Mtanzania (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-10-09.
  2. "Video: Mimi ndiye niliwashawishi SoundCity na MTV wawe na Top Ten za Afrika Mashariki – Diamond – Bongo5.com". bongo5.com. Iliwekwa mnamo 2022-10-09.
  3. D'jaro Arungu (TBC FM) na Tuzo za Zikomo (Zikomo Awards), iliwekwa mnamo 2022-10-09
  4. Lenzi Ya Mchezo (2015-05-24). "LENZI YA MICHEZO: Washindi wa tuzo za Watu 2015, hawa hapa". LENZI YA MICHEZO. Iliwekwa mnamo 2022-10-09.
  5. "MSIKILIZE D JARO ARUNGU WA TBC AKIIZUNGUMZIA TUZO ALIZO PATA KWENYE TUZO ZA WATU HAPA. - NGELANGELA NEWS". ngelangelanews.blogspot.com. Iliwekwa mnamo 2022-10-09.
  6. Salim Kikeke, D'jaro Arungu na Crew ya Mkasi ikiongea baada ya kushinda tuzo za watu, iliwekwa mnamo 2022-10-09

Viungo vya Nje