Instagram ni mtandao wa kijamii unaoruhusu mtumiaji kupata huduma ya kushirikisha picha za kawaida na za video mtandaoni.


Programu hii hutumika katika simu aidha za iPhone au mfumo uendeshaji wa Android. Programu inakupa fursa ya kuchukua picha na video, na kuzipitisha katika vichujio vyake ili itakate na kisha kuishirikisha na wale wanaokufuata. Vilevile inakupa fursa ya kushirikisha na mitandao mingine ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, JamiiTalk, Tumblr na Flickr.[1]

Mtandao huo uliundwa na Kevin Systrom na Mike Krieger na kutolewa rasmi tarehe 6 Oktoba 2010. Hivi sasa unamilikiwa na kampuni ya Facebook baada ya kununuliwa kwa dola za Kimarekani bilioni 1 Aprili 2012.

Baada ya kuanzishwa mwaka 2010, Instagram ilipata umaarufu mkubwa na kupata watumiaji milioni moja ndani ya miezi miwili, milioni 10 ndani ya mwaka mmoja na milioni 800 hadi Septemba 2017. Hadi Oktoba 2015 kulikuwa na picha bilioni 40 toka kwa watumiaji.

Historia

Instagram ni jukwaa maarufu la kushiriki picha na video ambalo lilianzishwa mnamo tarehe 6 Oktoba, mwaka 2010, na Kevin Systrom na Mike Krieger. Hapo awali, ilizinduliwa kwa jina la "Burbn" kama programu ya kushiriki maeneo na picha. Hata hivyo, baada ya muda, waligundua kuwa watumiaji walivutiwa zaidi na sehemu ya picha.

Mabadiliko yaliyofanywa na kuanzishwa kwa vipengele vipya yalisababisha kuzinduliwa upya kwa jukwaa hilo chini ya jina la Instagram mnamo Aprili mwaka 2012. Jina "Instagram" linatokana na maneno "instant camera" na telegram.

Instagram ilipata umaarufu haraka kutokana na muundo wake rahisi wa kushiriki picha na video na pia filamu za hadithi za muda mfupi (Instagram Stories) ambazo zinafutika baada ya masaa 24. Uzinduzi wa Instagram ulikuja wakati ambapo simu za mkononi zilikuwa zikipata umaarufu, na programu hii ilichangia kwa kiasi kikubwa katika mwelekeo wa kushiriki yaliyomo kwenye mitandao ya kijamii.

Mnamo mwaka 2012, Facebook ilinunua Instagram kwa dola bilioni moja, na tangu wakati huo, Instagram imekuwa ikiongeza mara kwa mara vipengele vipya, kama vile IGTV, Instagram Live, na vilevile kuboresha na kurekebisha jukwaa lake ili kukidhi mahitaji ya watumiaji wake wanaoendelea kuongezeka. Instagram imekuwa mojawapo ya majukwaa maarufu zaidi ya kijamii duniani, ikivutia watumiaji wengi na kutoa jukwaa kwa watu, makampuni, na wabunifu kushiriki yaliyomo na kujenga jamii mtandaoni.[2][3]

Matangazo

Kama ilivyo kwa mitandao mingine ya kijamii, Instagram inapata mamilioni ya fedha toka kwenye matangazo. Mnamo Oktoba 2013, Instagram ilianza jitihada za kupata fedha kupitia matangazo ya video na picha nchini Marekani. [4][5] Mnamo Juni 2014, Instagram ilitangaza ujio wa matangazo nchini Uingereza, Canada na Australia.[6]

Mnamo Mei 2016, Instagram ilitangaza uzinduzi wa zana mpya za akaunti za biashara, ikiwa ni pamoja na maelezo mafupi ya biashara, na uwezo wa kugeuza picha, video au maandishi kuwa matangazo moja kwa moja kutoka kwenye programu ya Instagram yenyewe.[7]

Mnamo Februari 2016, Instagram ilitangaza kwamba ilikuwa na matangazo 200,000.[8] Hii iliongezeka hadi kwa watangazaji wa kazi 500,000 mwezi Septemba 2016,[9] na milioni moja mwezi Machi 2017.[10]. Programu mbalimbali zimejitokeza kuwezesha watangazaji kujitanza kwenye Instagram kutokana na umaarufu wake.

Marejeo

  1. Frommer, Dan (Novemba 1, 2010). "Here's How To Use Instagram". Business Insider. Iliwekwa mnamo Mei 20, 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Siegler, MG (Oktoba 6, 2010). "Instagram Launches with the Hope of Igniting Communication Through Images". TechCrunch. AOL. Iliwekwa mnamo Aprili 8, 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Welcome to Instagram". Instagram. Oktoba 5, 2010. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-08-25. Iliwekwa mnamo Aprili 8, 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Panzarino, Matthew (Oktoba 3, 2013). "Instagram To Start Showing In-Feed Video And Image Ads To US Users". TechCrunch. AOL. Iliwekwa mnamo Aprili 23, 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Covert, Adrian (Oktoba 3, 2013). "Instagram: Now with ads". CNN Tech. CNN. Iliwekwa mnamo Aprili 23, 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Dove, Jackie (Juni 9, 2014). "Instagram will introduce ads in the UK, Canada and Australia 'later this year'". The Next Web. Iliwekwa mnamo Aprili 23, 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Perez, Sarah (Mei 31, 2016). "Instagram officially announces its new business tools". TechCrunch. AOL. Iliwekwa mnamo Aprili 23, 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Ha, Anthony (Februari 24, 2016). "There Are Now 200K Advertisers on Instagram". TechCrunch. AOL. Iliwekwa mnamo Aprili 23, 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. Ha, Anthony (Septemba 22, 2016). "And now there are 500K active advertisers on Instagram". TechCrunch. AOL. Iliwekwa mnamo Aprili 23, 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. Ingram, David (Machi 22, 2017). "Instagram says advertising base tops one million businesses". Reuters. Thomson Reuters. Iliwekwa mnamo Aprili 23, 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

  Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.