Daniel Kaminsky (Februari 7, 1979 - 23 Aprili 2021) alikuwa mtafiti wa usalama wa kompyuta wa Marekani. Alikuwa mwanzilishi mwenza na mwanasayansi mkuu wa WhiteOps, kampuni ya usalama wa kompyuta. Hapo awali alifanya kazi kwenye kampuni ya Cisco, Avaya, na IOActive, ambapo alikuwa mkurugenzi wa majaribio ya kupenya(Udukuzi wa mtandaoni)[1][2]. Gazeti la New York Times lilimtaja Kaminsky kuwa "mwokozi wa usalama wa Mtandao" na "Paul Revere wa kidijitali"[3].

Dan Kaminsky

Amezaliwa Februari 7, 1979
San Francisco
Amekufa 23 Aprili 2021
Nchi Marekani
Kazi yake alikuwa mtafiti wa usalama Tarakilishi
Cheo MWanasayansi

Maisha ya Awali

hariri

Daniel Kaminsky alizaliwa huko San Francisco mnamo Februari 7, 1979 , baba akijulikana kama Marshall Kaminsky na mama Trudy Maurer. Mama yake aliliambia gazeti la The New York Times kwamba baada ya baba yake kumnunulia kompyuta ya RadioShack akiwa na umri wa miaka minne, Kaminsky alianza kujifunza namna ya kutumia na kuandika lugha za kompyuta akiwa na umri wa miaka mitano. Akiwa na umri wa miaka 11, mama yake alipokea simu kutoka kwa msimamizi wa usalama wa serikali ambaye alimwambia kwamba Kaminsky alikuwa ametumia majaribio ya kupenya ili kuingilia kompyuta za kijeshi, na kwamba mtandao wa familia hiyo ungekatwa. Mama yake alijibu kwa kusema ikiwa mtandao wao utakatwa, angetoa tangazo katika shirika la habari la San Francisco lijulikanalo kama San Francisco Chronicle kutangaza ukweli kwamba mtoto wake wa miaka 11 anaweza kuvunja usalama wa kompyuta za kijeshi. Badala yake, suala la kufungiwa mtandao kwa siku tatu kwa Kaminsky ulijadiliwa.

Marejeo

hariri
  1. Singel, Ryan, "ISPs' Error Page Ads Let Hackers Hijack Entire Web, Researcher Discloses", Wired (kwa American English), ISSN 1059-1028, iliwekwa mnamo 2022-08-12
  2. "What is DNS rebinding attack? - Definition from WhatIs.com". SearchSecurity (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-08-12.
  3. "Daniel Kaminsky, Internet Security Savior, Dies at 42 - The New York …". archive.ph. 2021-04-29. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-29. Iliwekwa mnamo 2022-08-12.