Daniel Fernando Filmus (alizaliwa 3 Juni 1955 katika jiji la Buenos Aires) ni mwanasiasa na msomi wa Argentina. Hivi sasa, yeye ni Seneta wa Buenos Aires na alikuwa Waziri wa zamani wa Elimu, Sayansi na Teknolojia katika serikali ya Rais Néstor Kirchner.

Daniel Filmus akiwa Waziri wa Elimu katika nchi ya Argentina

Filmus alihusika, akiwa kijana, kwa muda mfupi katika mrengo wa Kikomunisti. Alisoma saikolojia na elimu ya jamii katika Chuo Kikuu cha Buenos Aires (UBA) na akashiriki katika siasa ya kiperonisti. Yeye alisaidia kuanzisha muungano unaodumu kuhusu haki za binadamu katika Chuo Kikuu cha Buenos Aires, akiwa mwanafunzi huko. Yeye alifuzu na kupata shahada ya daraja la pili katika Elimu kutoka Universidade Federal Fluminense katika jiji la Rio de Janeiro.

Filmus alikuwa mkuu wa Facultad Latinoamericana de Ciencias Sociales (FLASCO) na akawa msomi katika uwanja wa elimu huku akiandika vitabu kadhaa. Yeye aliingia sekta ya huduma za umma kama naibu waziri wa elimu wa waziri Carlos Grosso (yeye alikuwa alishiriki katika "ununuzi wa escuela", ambapo kipande cha ardhi cha shule kiliuzwa ili kuunda duka kubwa) na katika miaka ya 1990 alikuwa msaidizi wa Susana Decibe. Katika mwaka wa 2000, alikuwa waziri wa elimu katika jiji la Buenos Aires akiwa chini ya Anibal Ibarra, aliyemtaka Daniel kuwa naibu wake alipokuwa akigombea kiti cha rais katika uchaguzi wa 2003. Hata hivyo,kabla ya uchaguzi uliofanyika, Rais Kirchner alimwuliza Filmus kuwa Waziri wa Elimu. Yeye pia ni Profesa wa Elimu ya Jamii katika Chuo kikuu cha Buenos Aires.Filmus aligombea kiti cha meya wa Buenos Aires katika mwaka wa 2007, na akachukua nafsi ya pili baada ya kuhesabiwa kwa kura mnamo 24 Juni 2007 akishindwa na Mauricio Macri.

Baadaye katika mwaka wa 2007, alichaguliwa Seneta wa Buenos Aires na kuchukua ofisi yake katika mwezi wa Desemba 2007.

Marejeo hariri

  1. Daniel Filmus será el compañero de fórmula de Aníbal Ibarra Archived 10 Machi 2007 at the Wayback Machine.
  2. Bloomberg.com: Latin America

Viungo vya nje hariri