Democratic Party (Kenya)

Democratic Party (DP) au Chama cha Demokrasia ni chama cha kisiasa nchini Kenya. Kilianzishwa 1991 na Mwai Kibaki baada ya kuondoka kwake katika chama tawala cha KANU.

Chama kilikuwa na athira na uwezo hasa katika maeneo ya Wakikuyu. Kiliteua Kibaki kama mgombea wa uraisi mara mbili 1992 na 1998 bila kufaulu.

Mwaka 2002 DP iliingia katika maungano ya National Alliance Party of Kenya iliyoungana baadaye na LDP kuwa NARC iliyoshinda uchaguzi wa 2002. DP ilikuwa na wabunge 36 kati ya 126 wa NARC.

Kwa sasa hali yake haieleweki kwa sababu ilitangazwa mwaka 2006 kuwa sehemu ya chama kipya cha Kibaki yaani Party of National Unity.

Jinsi ilivyo na vyama vingi vya Kenya hakina muundo imara haijulikani ni watu wangapi wanoshiriki hali halisi katika mikutano yake kama iko.