Kenya African National Union

(Elekezwa kutoka KANU)

Kenya African National Union au KANU ni chama cha kisiasa nchini Kenya. KANU ilikuwa chama tawala cha nchi tangu uhuru katika mwaka 1963 hadi kushindwa katika uchaguzi wa 2002.

Chama cha uhuru

hariri

Chama kilianzishwa 1960 na wanasiasa waliyekuwa wanachama wa Kenya African Union ilichoanzishwa mwaka 1944 kwa jina la Kenya African Study Union. Jina likabadilishwa haraka kuwa "Kenya African Union" likabaki hivyo hadi 1952 KAU iliposimamishwa na serikali ya ukoloni. Mwenyekiti wa KAU ilipo ajiliwa alikuwa James Gichuru. Gichuru alipatia kiti chake cha uongozi Jomo Kenyatta wakati Kenyatta aliporudi Kenya baada ya miaka 20 ngambo. Gichuru angerudia tendo hili wakati alipochaguliwa kuongoza KANU ilipofufuliwa kupigania uchaguzi ambayo ingekuwa 1963. Kenyatta angeendelea kuongoza hiki chama tangu mwaka 1960 hadi kifo chake 1978. Tangu Oktoba 1978 Daniel Arap Moi akawa kiongozi wa chama.

Chama cha pekee

hariri

Katika uchaguzi wa 1963. KANU ilishinda vyama vya KADU na APP na kupata ruhusa ya kuunda serikali huru ya kwanza nchini Kenya. Mwaka iliyofuata wabunge wa hivi vyama walivuka sakafu na kujiunga na KANU. Kenya ikawa nchi ya utawala wa chama kimoja, yaani defacto. Mambo yaliendelea hivo hivo, isipokuwa muda mfupi kutoka 1966-69, mpaka 1982 mwaka katiba ya Kenya iliharirishwa kulingana na mfumo wa chama kimoja na KANU kuwa chama cha kisiasa cha pekee yaani dejure. Vyama vingine vilipigwa marufuku. Hali hii ilidumu hadi 1991 wakati serikali ya Moi ililazimishwa kukubali vyama vingi na badiliko la katiba tena.

Mfumo wa vyama vingi

hariri

Katika uchaguzi za 1992 na 1997 KANU ilifaulu kurudi kama chama kikubwa kwa sababu wapinzani wake walikosa umoja na kura za upinzani zilitawanyika kwa vyama mbalimbali kama vile Democratic Party of Kenya, Ford-Kenya, Ford-Asili na National Development Party of Kenya.

2001 Moi alipatana ushirikiano na Raila Odinga wa NDP aliyejiunga na serikali ya Moi kwanza kama waziri. Baadaye NDP ilijiunga na KANU na jina la chama cha pamoja likawa KANU Mpya (New KANU). Odinga akawa Katibu Mkuu.

Farakano la 2002 na upinzani

hariri

Mwaka 2002 Moi alipanga kukabidhi uongozi wa taifa mkononi mwa Uhuru Kenyatta aliye mtoto wa mzee Jomo Kenyatta kwa njia ya uchaguzi wa rais. Hii ilileta farakano ndani ya KANU. Kundi la Raila Odinga pamoja na wanaKANU wa miaki mingi waliondoka kwa sababu hawakuridhika na Kenyatta kuwa mgombea wa urais.

Wananchi wa Kenya walipendelea chama cha National Rainbow Coalition pamoja na mgombea wake Mwai Kibaki na KANU ilipata kura chache ikarudi bungeni kama chama cha upinzani.

Matatizo na kukaribiana na Kibaki

hariri

Wakati huu wa upinzani baada ya 2002 KANU iliona mafarakano mengi. Chama kilichobaki kiliongozwa na Uhuru Kenyatta lakini alipingwa na kundi chini ya Nicolas Biwott kilichojitenga kwa muda. 2006 wakajiunga na serikali ya umoja wa kitaifa cha Kibaki.

Kabla ya uchaguzi wa 2007 KANU iliunga mkono maungano ya Party of National Unity ya rais Kibaki ikimpigania Kibaki kama rais lakini kuwa na wagombea wake wa pekee. Kenyatta alitangaza ya kwamba KANU itadai cheo cha makamu wa rais.

Uchaguzi wa 2007

hariri

Katika uchaguzi wa 2007 KANU ilishika viti 11 bungeni. Wapinzani wa Kenyatta ndani ya chama walidhoofika baada ya Biwott kutofaulu kutetea nafasi yake bungeni.

Viungo vya Nje

hariri