Dennis Kipruto Kimetto
Dennis Kipruto Kimetto (alizaliwa 22 Januari 1984) ni mwanariadha wa masafa mrefu wa Kenya ambaye hukimbia katika mashindano ya kukimbia barabarani. Kimetto alikuwa na rekodi ya ulimwengu kwa marathoni ya wanaume na wakati ya 2:02:57. Yeye alikuwa na rekodi hiyo mpaka Eliud Kipchoge alipovunja rekodi mwaka wa 2018.
Sport | |
---|---|
Country | Kenya |
Sport | Riadha |
Event(s) | mbio za masafa marefu |
Maisha
haririKimetto anatoka mji wa Eldoret. Yeye alikulia kijijini katika mkoa wa bonde la ufa. “Nadhani kinachonitia motisha kuwa mpiganaji ni ukweli kwamba ninatoka katika hali ngumu. Ninajaribu kuhakikisha kuwa ninatimiza bora yangu ili niweze kusaidia familia yangu”.
Alikuwa mwanachama wa kikundi cha mafunzo kilichoongozwa na Geoffrey Mutai. Kimetto alipata ushindi mkubwa wa kwanza katika nusu marathoni wakati wa marathoni ya Nairobi mwaka 2011. Yeye alishinda na wakati ya 1:01:30.
Kimetto alipata umaarufu aliposhindana nje ya Kenya. Kimetto aliposhinda Nusu Marathon ya Berlin, umri wake uliripotiwa vibaya na watu walisema kwamba Kimetto ana miaka kumi pungufu kuliko alivyosema. Kwa hiyo watu walifikiri kwamba Kimetto alikuwa na rekodi ya ulimwengu ya vijana. Jina lake liliripotiwa kama Dennis Koech pia. Sababu ya yote hayo ilikuwa ni makosa kwenye pasipoti yake. Hii ilirekebishwa katika mashindano ya baadaye.
Kimetto aliendelea hadi kuvunja rekodi katika BIG 25 Berlin. Baadaye yeye alishindana na alikimbia kasi zaidi ya yeyote katika historia katika marathon ya kwanza yake. Tena huko Berlin, Kimetto alikimbia na Geoffery Mutai kwa sehemu kubwa ya mashindano na alimaliza sekunde moja nyuma ya Mutai na alikuwa na nafasi ya tano wenye kasi zaidi kuwahi kukimbia wakati huo. Baadhi ya waandishi wa habari walisema kwamba Kimetto alikaa nyuma ya Mutai wakati wa sehemu wa mwisho ya mashindano kwa sababu yeye alimtakia Mutai kupata Kombe la safu ya Marathon ya Ulimwengu ya watu wazima.
Mwaka 2013 Kimetto alivunja rekodi mbili katika kozi mbili katika Marathon ya Ulimwengu ya watu wazima. Alivunja rekodi katika mji wa Tokyo na wakati wa 2:06:50 na alivunja rekodi tena katika mji wa Chicago na wakati wa 2:03:45, wakati bora kabisa katika kozi ya ubora wa rekodi Marekani wakati huo. Mwaka 2014 mwezi wa tisa siku ya ishirini na nane, Kimetto alivunja rekodi ya ulimwengu katika Berlin Marathon na wakati wa 2:02:57 na akakuwa mwanaume wa kwanza alikimbia chini ya wakati 2:03. Isipokuwa wakati ya kuteremka na kusaidiwa sana na upepo katika Marathon ya Boston nusu wapili wa mbio yake ilikuwa haraka sana katika historia. Mwaka 2015 majira yake yalikuwa sio mazuri kama majira yaliopita kwa sababu yeye alimaliza tu Marathon ya London katika nafasi ya tatu. Kimetto hakumaliza IAAF Marathon ya Mashindano ya Dunia katika Beijing au Marathon ya Fukuoka kwa sababu alipata jeraha. Jeraha hili lilimfanya akose Olimpiki ya Rio na Marathon ya Chicago pia. Shinda za kuumia za Kimetto ziliendelea mwaka 2017, na jeraha la goti lilimfanya akose Marathon ya Boston. Kimetto hakuweza kumaliza Marathon ya Honolulu na Marathon ya Chicago tena mwaka huo huo.
Mafanikio
hariri- Matokeo yote kuhusu marathoni na nusu marathoni
Kenya | ||||
---|---|---|---|---|
2011 | Nairobi Half Marathon | Nairobi, Kenya | 1st | 1:01:30 |
RAK Half Marathon | Dubai, United Arab Emirates | 1st | 1:00:40 | |
2012 | Berlin Half Marathon | Berlin, Germany | 1st | 59:14 |
BIG 25 Berlin | Berlin, Germany | 1st | 1:11:18 | |
Berlin Marathon | Berlin, Germany | 2nd | 2:04:16 | |
2013 | Tokyo Marathon | Tokyo, Japan | 1st | 2:06:50 |
Chicago Marathon | Chicago, United States | 1st | 2:03:45 | |
2014 | Berlin Marathon | Berlin, Germany | 1st | 2:02:57 (WR) |
2015 | London Marathon | London, England | 3rd | 2:05:50 |
2016 | London Marathon | London, England | 9th | 2:11:44 |
2018 | Shanghai International Marathon | Shanghai, China | 10th | 2:14:54 |
Mashindano ya Dunia ya Marathoni | 2012 | 2013 | 2014 | 2015 | 2016 |
---|---|---|---|---|---|
Tokyo Marathon | - | 1st | - | - | - |
Boston Marathon | - | - | - | - | - |
London Marathon | - | - | - | 3rd | 9th |
Berlin Marathon | 2nd | - | 1st | - | - |
Chicago Marathon | - | 1st | - | - | - |
New York City Marathon | - | - | - | - | - |