Pasipoti (kwa Kiingereza passport) ni hati rasmi ambayo kwa kawaida inatolewa na serikali ya nchi na kumtambulisha mtu kama raia anayeruhusiwa kutoka na kurudi nchini. Ni hati muhimu kwa watu wanaovuka mipaka ya nchi.

Pasipoti ni mali ya nchi inayoitoa. Huwa na picha, jina na sahihi ya mtu aliyetolewa, pamoja na tarehe na mahali pa kuzaliwa kwake. Kuna nchi zinazoingiza pia habari za kimaumbile zinazofichwa kielektroniki.

Kati ya aina mbalimbali za pasipoti kuna

  • pasipoti ya kawaida
  • pasipoti ya kidiplomasia, inayotolewa hasa kwa watumishi waliopo kwenye balozi za nchi
  • pasipoti rasmi inayotolewa kwa watu wengine waliotumwa na serikali au kwa niaba ya serikali ya nchi yao bila ya kuwa na hali ya kidiplomasia.