Dennis Mitchell
Allen Dennis Mitchell (alizaliwa 20 Februari 1966) ni mwanamichezo wa zamani wa Marekani, mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio ya x 100 m katika Olimpiki ya 1992.
Rekodi za medali | ||
---|---|---|
Riadha ya Wanaume | ||
Anawakilisha nchi Marekani | ||
Michezo ya Olympiki | ||
Dhahabu | 1992,Barcelona | 4 x 100m |
Fedha | 1996,Atlanta | 4 x 100m |
Medali ya Shaba | 1992 Barcelona | 100m |
Mashindano ya Mabingwa wa Dunia | ||
Dhahabu | 1991 ,Tokyo | 4 x 100m |
Dhahabu | 1993 ,Stuttgart | 4 x 100m |
Medali ya Shaba | 1991, Tokyo | 100 m |
Medali ya Shaba | 1993 Stuttgart | 100 m |
Wasifu
haririAlizaliwa Havelock, Carolina Kaskazini, kocha wake Dennis Mitchell katika Chuo Kikuu cha Florida alikuwa Joe Walker(ambaye sasa yuko Ole Miss). Mitchell alichukua nafasi ya nne katika mbio ya 100m katika Olimpiki ya 1988 na akakosa kushinda medali katika mbio ya 4 x 100m kwa sababu timu ya Marekani ilitolewa katika mbio za mchujo.Timu yao ilitolewa baada ya Calvin Smith na Lee McNeill kubadilishana kijiti maalum wakiwa nje ya eneo maalum ya kubadilishana.
Katika mwaka wa 1989, Mitchell alishinda mbio ya mabingwa ya NCAA ya 200 m. Mwaka wa 1991, mwezi mmoja tu kabla ya Mashindano ya Mabingwa wa Dunia, Mitchell alikimbia rekodi yake ya kwanza ya ulimwengu katika mbio ya 4 x 100 m kwa muda wa 37.67 jijini Zürich. Katika {0}Mashindano ya Mabingwa wa Dunia,{/0}Mitchell alikuwa katika timu ya Marekani ya mbio 4 x 100m iliyoweka rekodi mpya ya dunia katika muda wa 37.50 katika fainali. Licha ya hayo,akashinda pia medali ya shaba katika mbio ya 100m.
Mwaka wa 1992, Mitchell alishinda taji lake la kwanza la Mashindano ya Kitaifa ya Mabingwa wa Marekani katika mbio ya 100m(alishinda taji hili tena katika miaka ya 1994 na 1996). Katika Olimpiki ya Barcelona, Mitchell alikimbia rekodi yake ya tatu ya dunia katika mbio ya 4 x 100m kwa muda wa 37.40 na kushinda medali ya shaba katika mbio ya 100m.
Katika Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya 1993,Mitchell alishinda medali ya shaba katika mbio ya 100m katika mashindano ya kimataifa.Alishinda ,pia,medali ya dhahabu ya tatu katika mbio ya 4 x 100m wakikimbia na muda sawa na rekodi yao ya 37.40s
Mitchell alishinda medali ya dhahabu katika mbio ya 100 m katika michezo ya Goodwill ya 1994 lakini akjiumiza katika mbio za mchujo za 100m katika Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya 1995. Katika Olimpiki ya 1996, Mitchell alichukua nafasi ya nne katika mbio ya 100 na akashinda medali ya fedha kama mwanachama wa timu ya 4 x 100.
Historia ya kutumia dawa haramu
haririMwaka wa 1998, Mitchell alikuwa amepigwa marufuku na IAAF kwa miaka miwili baada ya mtihani alionyesha viwango vya testosterone vilikuwa juu sana. Utetezi wake wa "chupa ya bia tano na kujamiiana na mke wake angalau mara nne ... ilikuwa sherehe yake ya siku ya kuzaliwa, mwanamke alihitaji kufurahishwa." ilikubaliwa na kamati ya Marekani ya Riadha lakini haikukubaliwa na IAAF. Dennis Mitchell alishiriki katika mashindano yake ya mwisho ya kimataifa katika Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya 2001,walipokuwa nambari ya kwanza lakini hawakutuzwa kwa sababu ya kashfa ya BALCO ya mmoja wao.
Tarehe 1 Mei 2008, ilitangazwa na serikali ya Marekani, katika kesi dhidi ya Trevor Graham, Bw. Mitchell na ,vilevile, Antonio Pettigrew kama mashahidi.Mitchell alikuwa anafaa kutoa ushuhuda dhidi ya Graham kuwa alijaribu kumdunga sindano ya homoni ya ukuaji haraka wa tishu.
Marejeo
haririViungo vya nje
hariri- Masters T&F 100 metres Dash All-Time Rankings Archived 25 Februari 2021 at the Wayback Machine. 10.11 (2001)
- Masters T&F 200 metres Dash All-Time Rankings Archived 17 Septemba 2018 at the Wayback Machine. 20.45 (2001)
Awards | ||
---|---|---|
Alitanguliwa na Michael Johnson |
Tuzo ya ESPY ya Riadha 1995 |
Akafuatiwa na Michael Johnson |