Stuttgart ni mji mkuu wa jimbo la Baden-Württemberg nchini Ujerumani wenye wakazi 590,000. Mji uko katika bonde la mto Neckar.

Nembo Ramani
Nembo la Stuttgart
Mahali pa Stuttgart katika Ujerumani
Mji wa Stuttgart.

Stuttgart ni mji mkubwa wa sita wa Ujerumani na kitovu cha kiuchumi cha Ujerumani kusini-magharibi. Makampuni makubwa kama vile Daimler, Porsche, Bosch, Hewlett-Packard, Kodak na IBM yana makao makuu yao kwa ajili ya Ujerumani au hata dunia nzima huko Stuttgart.

Historia hariri

Wakati wa Roma ya Kale palikuwa na boma la Waroma katika eneo la Stuttgart.

Mji wenyewe uliundwa mnamo mwaka 950 kama kituo cha kufuga farasi cha mtemi wa Swabia.

Tangu mwaka 1300 mji umekuwa mji mkuu wa watemi wa Württemberg walioendelea kujipatia cheo cha kifalme wakati wa vita za Napoleoni. Hivyo Stuttgart ikawa mji mkuu wa Ufalme wa Württemberg kuanzia mwaka 1805 hadi 1918. Baada ya mapinduzi ya mwaka 1918 Stuttgart ilikuwa mji mkuu wa jimbo la Württemberg na tangu mwaka 1952 wa Baden-Württemberg.

Mwaka 2006 Stuttgart ilikuwa mahali pa michezo katika mashindano ya soka duniani.

Watu mashuhuri hariri

 
Kitovu cha Stuttgart.

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Stuttgart kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.