Uganga wa meno

(Elekezwa kutoka Dentistry)

Uganga wa meno ni fani ya pekee katika elimu ya tiba. Hutekelezwa na daktari wa meno anayeelewa matatizo ya meno. Kazi yake ni kutambua magonjwa ya meno, kuyatibu na kuwashauri watu kuhusu namna za kutunza meno.

Kazi ya daktari wa meno wa kisasa

Daktari wa meno huwa na wasaidizi wenye elimu maalumu namna gani kusafisha meno na uwazi wa mdomo, wanaotengeneza misaada ya kurekebisha meno ya watoto wakati wa kukua au wanaojua kutengezea meno bandia. Kuna madaktari wa meno walioendelea kuwa wabingwa wa upasuaji wa meno na utaya.

Afya ya meno ni sehemu muhimu ya afya ya mwili kwa jumla. Magonjwa ya meno yanaweza kusababisha maumivu makali, kupunguza uwezo wa kula vyakula na kusababisha vidonda mdomoni ambavyo ni viingilio kwa magonwa mbalimbali. Kinyume chake kuna magonwa kadhaa yanayooyesha dalili yao hasa mdomoni ambako yanaweza kutambuliwa na daktari bingwa.

Madaktari wa meno walio wengi hufanya kazi katika kliniki ya binafsi kuna wengine waliopo hospitalini au katika taasisi za umma kama vile jeshini au gerezani.

Kutoa kwa jino, Uholanzi mnamo karne ya 17

Historia

hariri

Kutokana na utafiti wa akiolojia -hasa kwa kutazama mifupa kutoka makaburi ya kale- inajulikana ya kwamba huko katika utamaduni wa mto Indus kulikuwa na tiba ya meno katika karne ya 28 KK.[1]

Kutoka Misri ya Kale kuna papiri ya karne ya 16 KK yenye maelezo kuhusu tiba ya meno.[2]

Hata kama tiba ya meno ilijulikana tayari tangu kale wataalamu wa siku zile hawakuelewa bado ni nini inayosababisha magonwa mengi. Tangu siku za Sumer (miaka 5000 KK) "mnyoo" aliaminiwa kusababisha karisi (kuoza kwa meno)[3] na imani iliendelea kwa miaka mielfu.

Mbinu za kuwasaidia wenye matatizo ya meno zilijulikana pia tangu kale. Wataalamu wa Ugiriki ya Kale kama Hippokrates waliandika kuhusu namna ya kutoa meno magonjwa na kushika maneno katika utaya kwa msaada wa nyaya.[4].

Matumizi ya [maligamu]] (aloi za zebaki) kwa kujaza mashimo katika ina yalielezwa katik China ya Kale mnamo karne ya 7 BK [5].

Sayansi ya kisasa ilitokea katika kazi na maandiko ya daktari Mfaransa Pierre Fauchard (1678-1761) aliyetambua sukari kuwa sababu ya kuoza kwa meno, alibadilisha vifaa vya wafundi mbalimbali kwa matumizi katika tiba ya meno, [6], alieleza mbinu mbalimbali za kuingiza meno bandia mdomoni akatambua ya kwamba inawezekana kusahihisha hali ya meno yaliyokaa nje ya safu ya menu kwa kuyavuta kwa nyaya.

 
Vifaa vya utafiti katika uganga wa meno: kioo na kipima kidonda

Tiba ya meno

hariri

Matatizo ya afya ya meno yamekuwa muhimu katika afya ya umma ya kimataifa. Yanatokea mara nyingi na kuwa tatizo hasa kwa ajili ya watu maskini kote duniani wanaokosa pesa ya tiba. [7]

Daktari ataanza tiba wa mteja mpya kwa utafiti wa hali ya meno na uwazi wa mdomo hasa ya ufizi. Hapa msaidizi wake anaandika habari za hali ya kila jino kwenye kadi ya mteja itakayotunzwa katika ofisi ya daktari.

Ni hasa magonjwa mawili yanayohitaji kuangaliwa na madaktari wa meno

Mbinu za kawaida ni

  • kutengeneza meno magonjwa (kwa kusafisha karisi na kujaza shimo)
  • kutoa jino
  • tiba ya kanali ya neva ya jino

Wajibu muhimu wa daktari ya meno ni kuwashauri wateja kuhusu afya ya meno na sehemu hii huitwa "prophylaxis" yaani tiba ya kuzuia maradhi ya meno. Inahusu hasa usafi wa meno na mdomo, maana sehemu kubwa ya kuoza kwa meno husababishwa na uchafu unaobaki mdomoni na kati ya meno na kulisha bakteria zinazotengeneza asidi zinazoshambulia meno.

Ushauri mwingine utahusu chaguo la chakula maana

  • uhaba wa vitamini unadhoofisha meno na kuhatarisha fizi;
  • kutafuna vigumu kama kufungua jozi au chupa kwa meno inaweza kupasua jino

Marejeo

hariri
  1. Coppa, A. et al. 2006. Early Neolithic tradition of dentistry. Nature. Volume 440. 6 April 2006.
  2. https://web.archive.org/web/20050226100008/http://www.macalester.edu/~cuffel/ebers.htm Papiri Ebers
  3. History of Dentistry: Ancient Origins, hosted on the American Dental Association website. Page accessed 9 January 2007
  4. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-07-14. Iliwekwa mnamo 2014-07-04.
  5. Bjørklund G (1989). "The history of dental amalgam (in Norwegian)". Tidsskr nor Laegeforen 109 (34–36): 3582–3585. PMID 2694433.
  6. Bernhard Wolf Weinberger (1941). Pierre Fauchard, Surgeon-dentist: A Brief Account of the Beginning of Modern Dentistry, the First Dental Textbook, and Professional Life Two Hundred Years Ago. Pierre Fauchard Academy
  7. The World Oral Health Report 2003: continuous improvement of oral health in the 21st century – the approach of the WHO Global Oral Health Programme