Desonidi (Desonide) ni krimu ya steroidi inayotumika kutibu eczema, ugonjwa ya ngozi wa seborrheic, ugonjwa wa ngozi wa mguso, na hali ya seli za ngozi kujikusanya na kutengeneza gamba na mabaka makavu yanayowasha (psoriasis).[1] Inakuja kama krimu, dawa ya kuchua, losheni na povu.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuungua, maambukizi kwenye mifuko ambayo nywele hutokea (folliculitis), chunusi, na kukonda kwa ngozi.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha ugonjwa wa Cushing na sukari ya juu ya damu.[1] Madhara yake mengi ni ya kiwango cha chini.[2] Dawa hii ina nguvu ya chini hadi ya kati na imeainishwa kama kundi la kotikosteroidi la VI nchini Marekani.[1][3]

Desonidi iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1972.[1] Inapatikana kama dawa ya kawaida chini ya majina anuwai ya chapa.[4][1] Bomba la gramu 15 la 0.05% linagharimu takriban dola 15 za Kimarekani kufikia mwaka wa 2021.[4]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "Desonide Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 20 Septemba 2020. Iliwekwa mnamo 17 Julai 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Wong VK, Fuchs B, Lebwohl M (2004). "Overview on desonide 0.05%: a clinical safety profile". Journal of Drugs in Dermatology. 3 (4): 393–7. PMID 15303783.
  3. Bope, Edward T.; Kellerman, Rick D. (24 Novemba 2015). Conn's Current Therapy 2016 (kwa Kiingereza). Elsevier Health Sciences. uk. PT262. ISBN 978-0-323-35535-3. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 17 Julai 2021.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.0 4.1 "Desonide Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Juni 2019. Iliwekwa mnamo 17 Julai 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Desonidi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.