Diflorasoni diasetati

Diflorasoni diasetati (Diflorasone diacetate), inauzwa kwa jina la chapa Psorcon miongoni mwa mengine, ni steroidi inayopakwa juu ya ngozi.[1] Dawa hii inatumika kwa mwasho wa juu ya ngozi, hali ya seli za ngozi kujijenga na kutengeneza gamba na mabaka makavu yanayowasha (psoriasis), na ugonjwa wa mwasho wa ngozi unaotokana na mgusano.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuwashwa, maambukizi ya mifuko ambayo nywele hutokea (folliculitis), chunusi, kupungua kwa rangi ya ngozi, ugonjwa wa ngozi wa perioral, maambukizi, kuongezeka kwa nywele, na mistari ya rangi nyekundu ambayo kwa kawaida huonekana kwenye ngozi kutokana na kupata uzito haraka au kutokana na mabadiliko ya uzito (striae).[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha ugonjwa wa Cushing na athari za mzio.[1] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[1] Nguvu yake nchini Marekani imetiwa katika kundi la III.[2]

Diflorasoni diasetati iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1977.[1] Inapatikana kama dawa ya kawaida.[3] Nchini Marekani, bomba la gramu 30 hugharimu takriban dola 65 za Kimarekani kufikia mwaka wa 2021.[3]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Diflorasone Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 28 Desemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Topical Corticosteroids: Overview". 9 Julai 2021. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 28 Desemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 "Diflorasone Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Mei 2016. Iliwekwa mnamo 28 Desemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Diflorasoni diasetati kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.