Dola la Rakhaing
Dola la Rakhaing (pia Arakan) ni dola ndani ya taifa ya Myanmar (Burma) lililopo kwenye pwani la magahribi la nchi hii. Inapakana na Bangladesh.
Lina eneo la kilomita za mraba 36,762 na wakazi 3,118,963. Makao makuu yapo mjini Akjab unaoitwa pia Sittwe. Milima ya Arakan inafikia kimo cha mita 3,063 metres kwenye Victoria Peak. Baharii kuna visiwa vikubwa kadhaa.
Wakazi wa Rakhaing ni kutoka vikndi viwili hasa. Warakhaing wako wengi katika kusini. Katika kaskazini karibu na mpaka wa Bangladesh na kwenye pwani wakazi wengi ni Rohingya. Kuna pia makabila madogomadogo hasa mlimani wa nasaba na lugha tofauti.
Warakhaing ni Wabuddha wanatumia lugha iliyo karibu na Kiburma. Warohingya ni Waislamu na lugha yao ni karibu na Kibengali. Miaka ya nyuma kulikuwa na mapigano kati ya vikundi hivi viwili. Kuna ubaguzi mkali dhidi ya Warohingya wakishtakiwa eti si wananchi kweli bali wahamiaji kutoka Bara Hindi. Tangu 1983 waliondolewa uraya wa Burma wengi wamekuwa wakimbizi.