Dorothy Stang
Dorothy Mae Stang (7 Juni 1931 – 12 Februari 2005) [1] alikuwa mzaliwa wa Marekani, mtawa wa Brazil wa Shirika la Masista wa Notre Dame de Namur.
Aliuawa huko Anapu, katika jimbo la Pará, katika Bonde la Amazoni huko Brazil. Stang alikuwa amejitokeza wazi katika juhudi zake kwa ajili ya maskini na mazingira na hapo awali alipokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa wakataji miti na wamiliki wa ardhi. Kesi ya kutangazwa mtakatifu kama mtu wa imani na kielelezo cha utakatifu inaendelea ndani ya Kanisa Katoliki.
Marejeo
hariri- ↑ "Brazil: Bolsonaro supporter works to imprison Dorothy Stang's successor". Mongabay Environmental News (kwa American English). 2018-12-28. Iliwekwa mnamo 2019-11-19.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |