Dr. Rose Reuben ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania kwa sasa, pia ni mjumbe wa bodi ya THRDC.

Ni mtaalamu wa Jinsia, Maendeleo na Mawasiliano ambaye amewahi kufanya kazi kama mshauri wa kujitegemea anayelenga kuwashauri waandishi wa habari kuhusu uandishi wa habari za uchunguzi kuhusiana zaidi na haki za wanawake na watoto.

Amewahi pia kufanya kazi katika Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kama mwandishi mkuu wa habari, mhariri wa habari, mwandishi wa habari, mtayarishaji wa vipindi na mtangazaji.[1][2][3]

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dr. Rose Reuben kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.