Dubai Marina

Sehemu katika Dubai Marina


—— Jamii ya United Arab Emirates ——
Dubai Marina

Nchi United Arab Emirates
Emirate Dubai
Mji Dubai
Takwimu za Jamii
Ukubwa 4.9 million m²
Majamii Jirani Al Sufouh, Emirates Hills, Palm Jumeirah
Stesheni ya Reli ya Dubai Metro       Dubai Marina 
Nambari za Uratibu 25°4′52.86″N 55°8′38.67″E / 25.0813500°N 55.1440750°E / 25.0813500; 55.1440750

Dubai Marina ni eneo lililo mjini Dubai, ambao sasa unaitwa 'new Dubai'. Iko kwenye Interchange 5 karibu na Dubai Internet City na Dubai Media City. Upande mmoja wa eneo hili limemalizika kujengwa. Dubai Marina limebuniwa na kujengwa kama Concord Pacific Place iliyo kwenye False Creek mjini Vancouver, BC, nchini Canada.[1]

'Marina' yote imejengwa na kampuni ya ujenzi ya Emaar Properties iliyopo mjini Dubai. Sehemu ya kwanza ya Dubai Marina ipo kwenye ardhi ya eka 25 - ambapo kuna ghorofa sita za nyumba (Dubai Marina Towers) na majumba 64 ya anasa zilizo na mabustani kwenye dari zao. Ghorofa tatu kati ya hizo zimepewa majina kutokana na almasi: Al Mass, Fairooz na Murjan na ghorofa zingine tatu zimeitwa majina ya manukato ya Kiarabu: Mesk, Anbar na Al Yass.

Sehemu ya pili ya Dubai Marina ina takriban ghorofa 200 zikiwemo Al Majeera Towers na Al Sahab twin towers. Marina nyingine iliyojengwa duniani ni Marina del Rey mjini California, Marekani.

Ghorofa ndefu kabisa ni kama Pentominium, Ocean Heights, Damac Heights, Princess Tower, Marina 101, Marina 106, Elite Residence, na 23 Marina.

Hifadhi ya picha hariri

Viungo vya nje hariri

Marejeo hariri

  1. "BCBusiness: False Creek, Dubai". bcbusinessonline.ca. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-06-29. Iliwekwa mnamo 2009-02-21.