Falme za Kiarabu

(Elekezwa kutoka United Arab Emirates)


Falme za Kiarabu (kwa Kiarabu: الإمارات العربيّة المتّحدة; kwa Kiingereza United Arab Emirates) ni shirikisho la emirati au falme ndogo 7 katika kaskazini-mashariki ya Rasi ya Uarabuni kwenye mwambao wa ghuba ya Uajemi.

الإمارات العربيّة المتّحدة
Al-Imārāt al-ʿArabiyyah al-Muttaḥidah

Falme za Kiarabu
Bendera ya Falme za Kiarabu Nembo ya Falme za Kiarabu
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: none
Wimbo wa taifa: Ishy Bilady
Lokeshen ya Falme za Kiarabu
Mji mkuu Abu Dhabi
22°47′ N 54°37′ E
Mji mkubwa nchini Dubai
Lugha rasmi Kiarabu
Serikali Shirikisho, Ufalme
Khalifa bin Zayed Al Nahayan
M. bin Rashid Al Maktoum
Kuundwa kwa shirikisho
2 Desemba 1971
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
83,600 km² (ya 116)
--
Idadi ya watu
 - 2005 kadirio
 - 2005 sensa
 - Msongamano wa watu
 
4,496,000 (ya 116)
4,104,695 [1]
54/km² (ya 143)
Fedha Dirham (AED)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
GMT (UTC+4)
+4 (UTC)
Intaneti TLD .ae
Kodi ya simu +971

-


Shirikisho limepakana na Saudia na Omani kwenye nchi kavu; baharini kuna mipaka pia na Katar na Iran.

Mji mkuu ni Abu Dhabi na mji mkubwa ni Dubai.

Historia

hariri

Maeneo ya Falme za Kiarabu pamoja na Qatar na Bahrain yalikuwa nyumbani kwa makabila madogo na chifu zao.

Tangu mwaka 1820 walikuwa na mikataba na Uingereza walipoahidi kuachana na uharamia na kupokea ulinzi wa Uingereza. Ulinzi huu ulizuia uvamizi wa Saudia katika karne ya 20.

Falme hizo zilikuwa nchi lindwa chini ya Uingereza hadi mwaka 1971, ambapo madola hayo madogo yalipata uhuru. Saba kati yake yaliungana kwa jina la Falme za Kiarabu.

Wakazi

hariri

Mwaka 2013, wakazi wote walifikia milioni 9.2; kati yao, 1.4 raia na 7.8 wahamiaji. Hivyo asilimia 85 za wakazi ni wageni, kumbe wenyeji ni sehemu ndogo tu. Zaidi ya nusu ya wageni wanatoka katika nchi za Bara Hindi.

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kiarabu ambacho wenyeji wanakisema kwa lahaja maalumu ya Ghuba ya Uajemi. Tangu wakati wa ukoloni, Kiingereza kinatumika sana na kwa kawaida kinahitajika ili kupata kazi. Wahamiaji wanaendelea kutumia pia lugha zao za asili.

Uislamu ndio dini ya wenyeji (85% Wasuni na 15% Washia) na dini rasmi ya nchi, lakini kuna uhuru wa dini kwa wote, isipokuwa si uhuru wa kuieneza kwa wengine. Kati ya wakazi wote, Waislamu ni 76-77%, Wakristo (hasa Wakatoliki) ni 9-12%, Wahindu ni 4%, Wabuddha 2%, n.k.

Uchumi

hariri

Falme za Kiarabu zimekuwa nchi tajiri kutokana na akiba kubwa za mafuta ya petroli. Utajiri huo unapatikana kwa viwango tofautitofauti kati ya emirati zinazozunda shirikisho hili.

Abu Dhabi ni emirati mwanachama kubwa; ina pia kiasi kikubwa cha petroli na mapato makubwa kutokana na mauzo ya mafuta.

Emirati za Dubai na Sharjah zinazalisha pia petroli.

Emirati nyingine zinategemea msaada unaotolewa na Abu Dhabi hasa kutokana na mapato yake; pesa hizo zinasaidia ujenzi wa barabara na miundombinu kwa jumla.

Kazi nyingi za ofisini, viwandani, katika biashara na huduma zinatekelezwa na wageni ilhali wenyeji wanashika nafasi ya juu pekee; wengine wasio na vipaji vya kuongoza wanategemea malipo kutoka serikali.

Sheria ya nchi inasema ya kwamba makampuni yote nchini yanapaswa kuwa mikononi mwa raia wazalendo. Hali halisi inamaanisha ya kwamba wageni wanaunda kampuni wakimtafuta mwenyeji anayekubali sehemu ya mali na malipo ya kila mwaka bila kufanya kazi; lakini bila mwenyeji katika uongozi kampuni hairuhusiwi kuendesha shughuli zake kama ni kiwanda, duka au hoteli.

Makampuni kutoka nje yanaweza kupata leseni ya biashara kwa muda katika kanda za pekee bila kumshirikisha mwenyeji.

 
Ramani ya Falme za Kiarabu

Falme za shirikisho hili ni:

Jina Eneo (km²) Wakazi
mwisho wa 2006
Abu Dhabi 67.340 2.563.212
Umm al-Quwain 777 68.000
Fujairah 1.165 130.000
Ras al-Khaimah 1.684 214.000
Sharjah 2.590 699.000
Dubai 3.885 1.327.000
Ajmān 259 258.000

Tazama pia

hariri

Viungo vya nje

hariri
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Falme za Kiarabu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.