Dublin
Dublin (Kieire pia: Baile Átha Cliath = "Kijiji kwenye kivuko kwa mafunjo") ni mji mkuu wa Jamhuri ya Eire pia mji mkuu kwenye kisiwa cha Eire mwenye wakazi milioni 1.6 kwenye rundiko la jiji.
Jiji la Dublin | |
Majiranukta: 53°19′48″N 6°15′0″W / 53.33000°N 6.25000°W | |
Nchi | Eire |
---|---|
Mkoa | Leinster |
Wilaya | Dublin |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 505,739 |
Tovuti: www.dublincity.ie |
Jiografia
haririDublin iko kando la mdomo wa mto Liffey unapoishia katika Atlantiki kwenye pwani la mashariki la Eire.
Historia
haririWataalamu kadhaa hujaribu kuona uhusiano kati ya mji wa "Ebalana" uliotajwa na katika maandiko ya Ptolemeo mnamo 140 BK lakini hakuna uhakika kuhusu mahali pake.
Mji wa leo ulianzishwa kama kiji cha wavuvi kwa jina la „Áth Cliath“ na kando lake Wavikingi walijenga kijiji cha jirani cha „Dubh Linn“ ("matope mweusi"). Vijiji vikaungana na kuwa mji tangu 1172 kwa sababu Wanormandi baada ya kuvamia Eire kutoka Uingereza walianzisha makao makuu yao hapa. Katika kipindi hadi karne ya 16 Dublin ilikuwa kitovu cha eneo lililokuwa chini ya wafalme wa Uingereza kisiwani na tangu 1541 mji mkuu wa Ufalme wa Eire uliotawaliwa na mfalme wa Uingereza.
Baada ya muungano wa Uingereza na Eire katika Ufalme wa Muungano Dublin ilikuwa makao ya gavana mwingereza.
Uhuru wa Eire ulianza 1916 mjini Dublin kwenye uasi wa Pasaka. Kwenye Vita ya Uhuru ya Eire nyumba nyingi ziliharibiwa. Tangu uhuru wa 1922 Dublin ikawa mji mkuu.
Baada ya kujiunga kwa Eire na Umoja wa Ulaya Dublin imeendelea kukua na kuwa jiji ya Kiulaya. 1998 Dublin ilisheherekea sikukuu ya kumaliza miaka 1000.
Viungo vya Nje
haririPicha za Dublin
hariri-
Kanisa Kuu la Kristo Mfalme
-
Manisipaa ya Dublin
-
Nyumba ya forodha
-
Mnara wa Boma la Dublin
Makala hii kuhusu maeneo ya Ireland bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Dublin kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |