Edna Maskell

Mwanariadha wa Afrika Kusini na Zambia (1928-2018)

Edna Mary Therese Maskell (13 Aprili 1928 - 23 Juni 2018)[1] Ni mwanariadha wa kuruka viunzi ambaye alishinda medali ya dhahabu katika mita 80 kuruka viunzi akiwa mshindani wa Northern Rhodesia katika Michezo ya Madola na Jumuiya ya Uingereza ya mwaka 1954 huko Vancouver. Wakati wake bora binafsi ilikuwa sekunde 11.2. Pia alishinda medali ya shaba katika mbio za mita 100 katika Michezo ya Madola na Jumuiya ya Uingereza ya mwaka 1954 na alimaliza ya kumi katika kuruka mbali. Kabla ya hapo, alishiriki katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto ya 1952 huko Helsinki kwa niaba ya Afrika Kusini, akimaliza ya tano katika mbio zake za mita 80 kuruka viunzi.[2][3]

Marejeo

hariri
  1. https://www.olympedia.org/athletes/75233
  2. Edna Maskell at Sports reference.com. Retrieved 24 August 2013
  3. Old Miltonians Archived 12 Julai 2013 at the Wayback Machine. Retrieved 24 August 2013
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Edna Maskell kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.