Emily Greene Balch (8 Januari 18679 Januari 1961) alikuwa mtaalamu na mwandishi kutoka nchi ya Marekani. Tangu mwaka wa 1896 alifundisha masomo ya uchumi na ya jamii katika Chuo cha Wellesley, akapata uprofesa wa chuo kilekile mwaka wa 1913. Mwaka wa 1946, pamoja na John Mott alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel kwa Amani kwa ajili ya kazi yake na Ligi ya Wanawake ya Kimataifa kwa Amani na Uhuru.


Makala hii kuhusu mwandishi fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Emily Balch kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.