John Mott
John Raleigh Mott (25 Mei 1865 – 31 Januari 1955) alikuwa kiongozi wa YMCA na mashirikia mengine ya kikristo kutoka nchi ya Marekani.
Kuanzia mwaka wa 1895 hadi 1920 alikuwa katibu mkuu wa Chama cha Wanafunzi Wakristo Duniani.
Mwaka wa 1910, aliongoza Mkutano wa Misheni Duniani mjini Edinburgh unaohesabika kama mwanzo wa ekumeni katika karne ya 20.
Mwaka wa 1946, pamoja na Emily Balch alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani kwa ajili ya kazi yake ya kuanzisha na kuimarisha jumuiya za wanafunzi kwa ajili ya amani duniani.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |