Emirates Palace
Emirates Palace (Kiarabu: قصر الإمارات) ni hoteli ya starehe iliyopo mjini Abu Dhabi, UAE.
Ujenzi
haririIlifunguliwa mwezi Novemba 2005 lakini baadhi ya mikahawa na maduka hayakuwa wazi hadi 2006. Hoteli ilijengwa na inamilikiwa na serikali ya Abu Dhabi, na kwa sasa inasimamiwa na Kempinski Group.
Gharama ya kujenga hoteli hii ilikuwa dola bilioni 3. Emirates Palace ina upana wa 850,000 m². Kuna nafasi ya kuweka magari 2,500. Kuna mabwawa mawili ya kuogelea. Hoteli hii ina marina yake pamoja na kituo cha kushusha helikopta. Kulingana na gazeti la New York Times, Emirates Palace ni hoteli ya ghali zaidi kuwahi kujengwa [1]
Vipengele
haririNje
haririHoteli ina miviringo kama ya mskiti takriban 114 iliyo na urefu wa mita 60.
Ndani
haririVyumba vingi vimemaalizwa kwa dhahabu na marumaru. Eneo kuu la hoteli hii ina ukumbi wa marumaru pamoja na dhahabu. Ghorofa ya juu kabisa ina vyumba sita viavyotumiwa na maafisa au watawala muhimu wanaotembelea UAE. [1][2] Hoteli pia ina ukumbi mkubwa wa mkutano.
Vyumba na bei zake
haririKwa jumla, hoteli ina vyumba 302 na vyumba vya waheshimiwa 92. Vilevile, hoteli hii ina vyumba vingine 16 kwenye ghorofa ya sita na saba. Vyumba 22 vimetengewa wakuu wa nchi na wageni wao. Gharama ya kulala huanzia $400 kwa usiku mmoja kwenye Coral Room; na The Palace Grand Suite ni ghali zaidi - $11,500 per usiku. [3]
Viungo vya Nje
haririMarejeo
hariri- ↑ "Emirates Palace". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-10-30. Iliwekwa mnamo 2010-01-05.
- ↑ "Emirates Palace". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-10-30. Iliwekwa mnamo 2010-01-05.
- ↑ "Emirates Palace Hotel". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-12-31. Iliwekwa mnamo 2010-01-05.