Hoteli
Hoteli mojawapo.

Hoteli (kutoka neno la Kiingereza hotel linalotokana na lile la Kifaransa hôtel ambalo, sawa na neno "hospitali", lina asili katika Kilatini hospes, yaani mgeni) ni jengo kubwa lenye vyumba vingi, ambapo watu wanaweza kulala wakati hawapo nyumbani.

Wenye sehemu hizo wanakodisha chumba kwa siku yoyote. Wanatoa vyumba vya kulala, na kwa kawaida hata chakula, hatimaye kwa ajili ya huduma hizo hutaka pesa, ambazo kiasi chake hutegemea ubora wa jengo.

Pia kuna hoteli ambapo mikutano hufanyika.

Moteli ni hoteli hasa kwa madereva, waendesha pikipiki n.k.

ThreeCoins.svg Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hoteli kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.