Emma Miloyo

Msanifu wa Majengo wa nchini Kenya

Emma Miloyo (alizaliwa Nairobi, 1981) ni mbunifu wa nchini Kenya, ambaye aliripotiwa, mwaka wa 2017,[1] kuwa rais wa kwanza mwanamke wa Chama cha Usanifu wa Majengo cha Kenya. Anahudumu kama Rais wa kwanza mwanamke wa Muungano wa Usanifu wa Kenya tangu 2017. Mnamo Oktoba 2016, Archinect.com ilimworodhesha miongoni mwa Wasanifu watano Wanaochipuka wa Kike wa Afrika Mashariki, katika eneo la Nchi za Maziwa Makuu ya Afrika.[2]

Maisha ya awali na elimu

hariri

Emma Miloyo alizaliwa na kukulia Nairobi. Alisomea Shule ya Msingi ya Loreto Msongari, kabla ya kuhamia Shule ya Upili ya Kenya. [3] Alisomea usanifu katika Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta, na kuhitimu Shahada ya Usanifu mnamo 2006.[4] akiwa mwanamke wa kwanza kuhitimu kutoka chuo hicho na kupata shahada ya kwanza ya heshima ya usanifu.

Kufikia Oktoba 2018, alikuwa mshirika katika kampuni ya usanifu, Design Source, ambayo aliianzisha mnamo Januari 2007, nje ya chuo kikuu. Kampuni hii ina ofisi Nairobi na Mombasa.Alikuwa mwanachama mwanzilishi wa bodi ya Konza Technology City Board.

Mnamo Juni 2015, alichaguliwa kama Makamu wa Rais wa Muungano wa Usanifu wa Kenya, akihudumu katika wadhifa huo hadi Februari 2017.Alikua rais wa kwanza mwanamke wa Muungano wa Usanifu wa Kenya mnamo Machi 2017.

Emma ana nia ya kuhamasisha wanawake wachanga kuona usanifu kama chaguo bora la kazi. Ili kusaidia vijana, anajitolea wakati wake kusaidia wasichana walio katika umaskini kuhudhuria shule kupitia Mfuko wa Udhamini wa Elimu wa Zamani wa Bomarian na ni Mwanachama mwanzilishi wa Bodi ya WIRE (Wanawake katika Majengo).[5]

Maisha binafsi

hariri

Emma Miloyo ameolewa na Chris Naicca, mbunifu mwenzake na mwanafunzi mwenzake katika chuo kikuu. Kwa pamoja, wamezaa watoto watatu. Miloyo na Naicca ni washirika wa Design Source Limited, kampuni ya usanifu waliyoianzisha mwaka wa 2007.[6] Miloyo and Naicca are partners in Design Source Limited, the architectural firm they co-founded in 2007.[7]

Utambuzi

hariri

Business Daily Africa ilimworodhesha kama, mmoja wa Wanawake 40 bora wa Kenya chini ya 40 katika Business Daily Africa mwaka wa 2011 na 2018.

Marejeo

hariri
  1. BuyRentKenya (15 Septemba 2017). "Meet Emma Miloyo: Kenya's First Female Architect". Nairobi: BuyRentKenya.com. Iliwekwa mnamo 16 Februari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. https://ke.linkedin.com/in/emma-miloyo-52315b4
  3. Buy Rent Kenya (15 Septemba 2017). "Meet Emma Miloyo: Kenya's First Female Architect". Nairobi: Buyrentkenya.com. Iliwekwa mnamo 6 Oktoba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Miloyo, Emma (6 Oktoba 2018). "Emma Miloyo: President at The Architectural Association of Kenya". Linkedin.com. Iliwekwa mnamo 6 Oktoba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Kahongeh, James (7 Julai 2017). "Mentorship will take you places..." Daily Nation. Nairobi. Iliwekwa mnamo 6 Oktoba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Business Daily Staff (Septemba 2018). "Top 40 Under 40 Women In Kenya 2018" (PDF). Business Daily Africa. Nairobi. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-09-29. Iliwekwa mnamo 6 Oktoba 2018. {{cite web}}: |author= has generic name (help); More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. JAA (28 Machi 2017). "Emma Miloyo: Part 28 of a month-long celebration of Women's History Month". Matters of Taste. Iliwekwa mnamo 6 Oktoba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Emma Miloyo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.