"Eneka" ni jina la wimbo uliotoka tarehe 10 Julai, 2017 kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania - Diamond Platnumz. Wimbo unatoka katika albamu ya A Boy From Tandale na wa sita kutolewa kama single kutoka katika albamu hiyo. Wimbo umetayarishwa na Laizer Classic kupitia studio za Wasafi Records. Awali baada ya kutoka, kulivuma taarifa ya kwamba mapigo ya wimbo yanafanana sana na wa Davido "Fall" uliotoka kabla ya Eneka.

“Eneka”
“Eneka” cover
Kava ya Eneka
Single ya Diamond Platnumz
kutoka katika albamu ya A Boy from Tandale
Imetolewa 10 Julai, 2017
Muundo Upakuzi wa mtandaoni
Imerekodiwa 2017
Aina Bongo Flava, Afro-pop
Urefu 3:34
Studio Wasafi Records
Mtunzi Diamond Platnumz
Mtayarishaji Laizer Classic
Mwenendo wa single za Diamond Platnumz
"Fire"
"(2017)"
"Eneka"
"(2017)"
"Hallelujah"
(2017)

Kwa taarifa hizo, mtayarishaji wa wimbo huu "Laizer Classic" alilamizika kutetea hoja hii kwa kupitia mtandao wa Millard Ayo na kusema: "Sioni ajabu kwamba mtu akisema hii imefanana…mi ninachojali ni kwamba watu watapokeaje nyimbo, itapendwa au itafanya vizuri. Hicho ndicho ninachokiangalia zaidi." Katika mahojiano, Laizer alikiri kama sehemu kubwa ya utengenezaji wa nyimbo hufuata mtindo wa Kinigeria na wao walitangulia hivyo lazima utafanana na wao.[1]

Lengo la Chibu kwa wimbo huu ilikuwa kupata ladha ya kimataifa na kusukuma gurudumu la Bongo Flava nje ya nchi. Alitoa nyimbo mbili kwa pamoja, I Miss You ukiwa Bongo Flava halisi huku Eneka ikiwa Afro-pop kwa ajili ya kimataifa.[2]

Huu ndio wimbo wa kwanza kwa Chibu kufanya kazi na mwongozaji Sesan kutoka Nigeria. Video ilifanywa nchini Afrika Kusini.[3]

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

Viungo vya Nje hariri