Europe
Europe ni bendi ya muziki wa rock kutoka nchini Uswidi, ambayo ilianzishwa mjini Upplands Väsby mnamo 1979 ikiwa chini ya jina la Force. Bendi ilianzishwa na mwimbaji Joey Tempest na mpiga gitaa John Norum. Muziki mzima wa bendi hii hutumia metali zito na elementi kadhaa za hard rock au rock ya kigumu. Tangu kuanzishwa kwake, Europe imepata kutoa albamu nane za studio, tatu albamu za live, tatu kompilesheni na video nane.
Europe | |
---|---|
Europe performing in Lakselv, Norway 2008.
| |
Maelezo ya awali | |
Asili yake | Upplands Väsby, Uswidi |
Aina ya muziki | Hard rock, Glam metal |
Miaka ya kazi | 1979–1992 1999 (kuungana tena) 2003–mpaka sasa |
Studio | Hot Records, Epic, Sanctuary |
Ame/Wameshirikiana na | Tone Norum, Easy Action, Dokken, Glenn Hughes, Brazen Abbot, Clockwise, Last Autumn's Dream |
Tovuti | www.europetheband.com |
Wanachama wa sasa | |
Joey Tempest John Norum John Levén Mic Michaeli Ian Haugland | |
Wanachama wa zamani | |
Kee Marcello Tony Reno Peter Olsson Marcel Jacob |