Ezekiel Mphahlele

Mwandishi na mchapishaji wa Afrika Kusini

Ezekiel "Es'kia" Mpahlele (17 Desemba 1919 - 27 Oktoba 2008) alikuwa mwandishi wa Afrika Kusini. Aliandika hadithi fupi, riwaya na insha za kiuhakiki. Mwaka wa 1957 alihama Afrika Kusini kwa sababu za kisiasa akaishi nchi mbalimbali, baadhi yao Nigeria, Zambia na Marekani. Mwaka wa 1978 aliruhusiwa kurudi Afrika Kusini akawa profesa wa fasihi katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand.

Maandishi yake hariri

  • Down Second Avenue (tawasifu, 1959)
  • The African Image (andika la kiuhakiki, 1962, toleo la pili 1974)
  • The Wanderers (riwaya, 1971)
  • Voices in the Whirlwind (insha za kiuhakiki, 1972)
  • Chirundu (riwaya, 1979)
  • The Unbroken Song (hadithi fupi na mashairi, 1981)
  • Exiles and Homecomings (tawasifu, 1983)
  • Afrika My Music, 1957-1983 (tawasifu, 1984)

Angalia pia hariri

Marejeo hariri

  • Chapman, Michael. 2003. Southern African Literatures, University of Natal Press. ISBN 1-86914-028-1
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ezekiel Mphahlele kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.