Fatma Salman Kotan

Fatma Salman Kotan ni Mbuge wa Uturuki wa mji wa Ağrı kwa kupitia chama tawala cha AKP.

Alizaliwa mjini Doğubeyazıt, Ağrı mnamo mwaka wa 1970, Fatma Kotan ni mhasibu. Amesomea masuala wa uchumi katika Chuo Kikuu cha Ataturk cha mjini Erzurum.

Alizungumza mbele ya Jumuia ya Makabaila Wanawake wa Uturuki mnamo mwezi Agosti katika mwaka wa 2007 na kutoa hadithi ya maisha yake ni kama ifuatavyo:

Mama yangu alikuwa mke wa pili kwa baba yangu. Katika moja kati ya dunia yao endapo mwanaume atakuwa tajiri au anawezo basi ataoa zaidi ya mara moja. Mama yangu alifariki kwa sabab ya baba yangu kwa kumlasimisha kumzalia mtoto wa kiume. Hapo mimi nilikuwa mtoto wa pili kuzaliwa katika familia.

Daktari alimweleza mama kwamba ni hatari kwa yeye kuzaa mtoto wa tatu, lakini mama akatueleza kwamba anataka kumfurahisha baba yenu Sheikh Ahmet Salman, na kuendeleza mlolongo mwingine wa uzazi ili azae mtoto wa kiume. Daktari akamweleza itakuwa shughuli kupata ujauzito, lakini mama hakumsikiliza.

Mama akaendeleza kusema kwamba, mtoto pekee wa kiume ndiyo atakaye mfurahisha Sheikh Ahmet Salman. Baada uzaidi, mama akazaa mtoto mwingine wa kike. Miaka miwili baadaye mama akafariki dunia.

Tangu utoto wangu nilikuwa nacho hicho kitu akilini kwamba sio mwanaume tu ambaye anaweza kuishirikia familia ya Sheikh Ahmet Salman, hata mwanamke pia anaweza kufanya hivyo. Na ndiyomaana nimekuwa mwanamke wa kwanza katika famili yetu kwenda shule.

Nimejishughulisha na masuala ya siasa na biashara. Nilikuwa jua tu endapo nikifanya hivyo itakuwa ni mfano kwa wanawake wengine kufanya kama jinsi nilivyofanya mimi. Siku ya ufunguzi wa kiwanda cha matofali katika eneo hilo nilionyesha kwamba mwanamke anaweza kufanya kazi katika sehemu ya vumbi na matope.

Sasa hivi idadi ya wanawake wanofanya kazi katika eneo hilo inaongezeka. Lakini endapo hatuto uangusha ubaguzi wa kijinsia hata kidogo, basi ujue Uturuki ya mwaka wa 2007 itabaki kama ile ya mwaka wa 1970.[1]

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fatma Salman Kotan kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.