Federico Santiago Valverde Dipetta (alizaliwa 22 Julai 1998)[1][1] ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka Uruguay ambaye anacheza kama kiungo wa kati wa klabu ya La Liga Real Madrid na timu ya taifa ya Uruguay. Anajulikana kwa kasi, stamina na uwezo wake mkubwa wa kupiga mashuti, anachukuliwa kuwa mmoja wa viungo bora zaidi duniani. Hasa kama kiungo wa kati, pia ana uwezo wa kucheza kama kiungo mkabaji, winga wa kulia na kwa mara chache beki wa kulia.[2][3]

Valverde mnamo 2024

Valverde alianza kazi yake kama mchezaji wa mpira wa miguu akiwa na Peñarol mnamo 2015, alishinda kombe la ligi ya Uruguayan Primera División katika msimu wake wa kwanza. Mnamo 2016, alijiunga na Real Madrid,[4] Valverde alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa kwenye timu ya taifa Uruguay mnamo 2017 na tangu wakati huo amewakilisha nchi yake kwenye Copa América ya 2019, Copa América 2021, na Kombe la Dunia la FIFA 2022. Ameshinda tuzo ya mpira wa fedha kwenye Kombe la Dunia la Klabu ya FIFA mnamo 2022[5] na alijumuishwa katika timu ya msimu ya La Liga mnamo 2023.

Marejeo hariri

  1. https://web.archive.org/web/20200615194220/http://actas.rfef.es/actas/RFEF_CmpActa1?cod_primaria=1000144&CodActa=2782
  2. "Fede Valverde's transformation into one of the best midfielders in the world". MARCA (kwa Kiingereza). 2022-10-17. Iliwekwa mnamo 2024-04-18. 
  3. https://www.fifa.com/fifaplus/en/articles/the-tale-of-the-boy-who-didnt-want-to-run
  4. Víctor Mata, @VictorVMG13, Adapted by Harry De Cosemo (2016-07-27). "Real Madrid sign up starlet Valverde". MARCA English (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-18. 
  5. Pablo Polo, Madrid (2017-06-12). "U20 World Cup displays convince Real Madrid of Valverde talent". MARCA in English (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-18. 
  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Federico Valverde kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.