Fentanili

(Elekezwa kutoka Fentanyl)

Fentanili (kwa Kiingereza: Fentanyl au fentanil) ni afyuni inayotumika kama dawa ya kutuliza maumivu na pamoja na dawa nyingine za ganzi.[1] Fentanili pia hutumika kama dawa ya kujiburudisha, mara nyingi huchanganywa na heroini au kokeini.[2] Ina mwanzo wa haraka na athari zake kwa ujumla hudumu chini ya masaa mawili.[1] Kimatabibu, fentanili hutumiwa kupitia kudungwa sindano, dawa ya kupuliza puani, kiraka cha ngozi, au kufyonzwa kupitia shavu kama lozenji au tembe.[1][3]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kutapika, kuvimbiwa choo, kutuliza, kuchanganyikiwa, kuona njozi, na majeraha yanayohusiana na uratibu duni.[1][4] Madhara yake makubwa yanaweza kujumuisha kupungua kwa kupumua, ugonjwa wa serotonini, shinikizo la chini la damu, uraibu, au kukosa ufahamu.[1][4] Fentanili hufanya kazi hasa kwa kuwezesha vipokezi vya afyuni μ (μ-opioid).[1] Ina nguvu karibu mara 100 kuliko Mofini (morphine), na baadhi ya analogi kama vile karfenantili (carfentanil) zina nguvu karibu mara 10,000 zaidi yake.[5]

Fentanili ilitengenezwa kwa mara ya kwanza na Paul Janssen mwaka wa 1960 na kuidhinishwa kwa matumizi ya matibabu nchini Marekani mwaka wa 1968.[1][6] Mnamo mwaka wa 2015, kilogram 1 600 (lb 3 500) zilitumika katika huduma za kiafya duniani kote.[7] Kufikia mwaka wa 2017, fentanili ilikuwa afyuni ya sintetiki iliyotumiwa sana katika dawa.[8] Aina kali ya Fentanilli ya maumivu ya saratani iko kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika la Afya Ulimwenguni.[9] Katika mwaka wa 2016, fentanili na madawa mengine yenye muundo sawa nayo zilikuwa ndizo sababu ya kawaida ya vifo vya kupita kiasi cha dawa nchini Merika kwa zaidi ya 20,000, karibu nusu ya vifo vyote vinavyohusiana na afyuni.[10][11] Vingi vya vifo hivi vya kupita kiasi cha dawa vilitokana na fentanili iliyotengenezwa kinyume cha sheria.[12]

Kwa kichupa cha mikrogramu 100, wastani wa gharama ya jumla katika nchi zinazoendelea ilikuwa US$ 0.66 mwaka wa 2015.[13] Mnamo mwaka wa 2017, bei yake nchini Marekani ili US$ 0.49 kwa kiasi hicho hicho.[14] Nchini Marekani, tembe ya mikrogramu 800 ilikuwa ghali mara 6.75 zaidi ya mwaka wa 2020 kuliko lozenji (mchanganyiko wa sukari na protini ya asili, mumunyifu iliyoundwa kutoa dawa huku ikiyeyuka polepole mdomoni).[15] [16] Mnamo mwaka wa 2017, ilikuwa dawa ya 250 inayoagizwa zaidi nchini Marekani, ikiwa na maagizo zaidi ya milioni 1.7.[17][18]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "Fentanyl, Fentanyl Citrate, Fentanyl Hydrochloride". The American Society of Health-System Pharmacists. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Desemba 2017. Iliwekwa mnamo 8 Desemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Fentanyl Drug Overdose". CDC Injury Center. 29 Agosti 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 15 Desemba 2017. Iliwekwa mnamo 14 Desemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "tablets". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-07-31.
  4. 4.0 4.1 "Fentanyl Side Effects in Detail - Drugs.com". 
  5. "Commission on Narcotic Drugs takes decisive step to help prevent deadly fentanyl overdoses". Commission on Narcotic Drugs, United Nations Office on Drugs and Crime. 16 Machi 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 20 Machi 2017. Iliwekwa mnamo 19 Machi 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Stanley TH (Aprili 1992). "The history and development of the fentanyl series". Journal of Pain and Symptom Management. 7 (3 Suppl): S3-7. doi:10.1016/0885-3924(92)90047-L. PMID 1517629.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Narcotic Drugs Estimated World Requirements for 2017 Statistics for 2015 (PDF). New York: United Nations. 2016. uk. 40. ISBN 978-92-1-048163-2. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 22 Oktoba 2017. Iliwekwa mnamo 14 Desemba 2017.
  8. "Fentanyl And Analogues". LverTox. 16 Oktoba 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Januari 2017. Iliwekwa mnamo 14 Desemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. World Health Organization (2019). World Health Organization model list of essential medicines: 21st list 2019. Geneva: World Health Organization. hdl:10665/325771. WHO/MVP/EMP/IAU/2019.06. License: CC BY-NC-SA 3.0 IGO.
  10. "Overdose Death Rates". National Institute on Drug Abuse. 15 Septemba 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Desemba 2017. Iliwekwa mnamo 14 Desemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. Hedegaard H, Bastian BA, Trinidad JP, Spencer M, Warner M (Desemba 2018). "Drugs Most Frequently Involved in Drug Overdose Deaths: United States, 2011-2016". National Vital Statistics Reports. 67 (9): 1–14. PMID 30707673.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. "Fentanyl Drug Overdose". CDC. 21 Desemba 2018. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 15 Desemba 2017. Iliwekwa mnamo 28 Aprili 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  13. "Single Drug Information". International Medical Products Price Guide. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 15 Desemba 2017. Iliwekwa mnamo 14 Desemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  14. "NADAC as of 2017-12-13". Centers for Medicare and Medicaid Services. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Desemba 2017. Iliwekwa mnamo 14 Desemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  15. "Fentanyl Buccal". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-07-31.
  16. "Fentanyl Citrate Generic Actiq". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 31 Julai 2020. Iliwekwa mnamo 27 Mei 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  17. "The Top 300 of 2020". ClinCalc. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Februari 2021. Iliwekwa mnamo 29 Aprili 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  18. "Fentanyl - Drug Usage Statistics". ClinCalc. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Aprili 2020. Iliwekwa mnamo 29 Aprili 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)