Fernando Avendaño
Fernando Avendaño au Fernando de Avendaño (Lima, Peru, 1600 – Lima, 1665) alikuwa kasisi wa Kikatoliki.
Alifariki muda mfupi baada ya kuteuliwa kuwa Askofu wa Santiago, Chile.
Avendaño alijulikana kwa uchunguzi wake wa mabaki ya mila na desturi za asili za Waindio wa Peru. Vipande vya maelezo yake kuhusu mada hiyo vimehifadhiwa katika kazi ya Pablo José Arriaga.
Mahubiri yake, yaliyofahamika kama Sermones de los misterios de nuestra santa Fe católica, yalitolewa kwa lugha ya Kiquechua na kuchapishwa pamoja na tafsiri ya Kihispania mnamo mwaka 1649 kwa amri ya Askofu Mkuu wa Lima, Petro Villagomez.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |