Fikra za Xi Jinping
Fikra za Xi Jinping juu ya Ujamaa Wenye Sura za Kichina wa Zama Mpya (Kichina kilichorahisishwa: 习近平 新 时代 中国 特色 社会主义 思想; Kichina cha jadi: ☞近平 新 時代 中國 特色 社會主義 思想), ni nadharia ya kisiasa inayotokana na rais wa China na Xi Jinping Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China.
Inaaminika kuwa Fikra za Xi Jinping, ambazo zina kanuni 14, zitaingizwa katika katiba ya chama tawala. Xi Jinping atakuwa ni kiongozi wa kwanza ambaye jina lake linahusishwa na natharia ya kisiasa toka enzi za Deng Xiaoping ambaye alijiuzulu mwaka 1989. Kiongozi mwingine kuwa na sifa hii ni Mao Zedong.
Kwa mujibu wa shirika la habari la China, Xinhua, fikra hizi ni moja ya mambo makubwa katika mkutano wa 19 wa chama tawala wa 2017 ambao hufanyika kila baada ya miaka 5.[1]
Marejeo
hariri= Viungo vya Nje
hariri
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |