Mao Zedong (26 Desemba 1893 - 9 Septemba 1976) alikuwa kiongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China tangu 1935 hadi kifo chake na pia kiongozi mkuu wa China tangu 1949.

Mao Zedong mwaka 1959.

Aliongoza wakomunisti katika vita dhidi ya jeshi la Japan wakati wa vita kuu ya pili ya dunia na katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya China dhidi ya serikali ya chama cha Kuomintang iliyoongozwa na Chiang Kaisheck vilipomalizika kwa ushindi wake mwaka 1949.

Mao alibadilisha itikadi ya Umarx-Ulenin kwa mahitaji ya wakomunisti wa China. Mwelekeo wake huitwa "Umao".

Alijaribu kujenga ukomunisti nchini kwa kutegemea wakulima kuliko wanafayakazi jinsi ilivyokuwa itikadi ya kawaida ya Ukomunisti.

Siasa yake ya kiuchumi ilisababisha njaa na vifo vingi. Kwa jumla ni watu milioni 35 hadi 70 wanaokadiriwa walikufa kutokana na njaa au mateso chini ya Mao.

Dhidi ya wapinzani wake ndani ya chama alianzisha tangu mwaka 1966 "mapinduzi ya utamaduni" iliyoharibu mapokeo mengi na sehemu kubwa ya urithi wa kihistoria ya China.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mao Zedong kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.