Filamu za Korea Kusini

Filamu kutoka Korea Kusini (kwa Kikorea: 한국 드라마, han-guk drama) huitwa K-drama pia. Filamu za Kikorea ni tamthiliya za televisheni za Kikorea ambazo zimetengenezewa Korea Kusini.  

Filamu hizi zinajulikana ulimwengu kote, mahsusi katika Asia zaidi, kutokana na kuenea kwa utamaduni maarufu wa Kikorea na kupatikana kwa njia nyingi kupitia huduma za intaneti, ambazo mara nyingi hutoa tafsiri katika lugha nyingi. Filamu nyingi za Kikorea zimetafsiriwa kwa lugha tofauti tofauti, na baadhi yake zimekuwa na ushawishi mkubwa katika mataifa mengine. Katika nchi nyingine, chaneli za televisheni zimekuwa zikionyesha filamu za Kikorea. Kwa mfano, watu zaidi ya milioni 142 walitazama Squid Game (2021) (kwa Kikorea: 오징어 게임, O-jing-uh geim) na hii ikawa filamu iliyotazamwa zaidi kupitia Netflix. [1]

Mtindo

hariri

Fliamu za Kikorea zinavutia hisia za kimataifa kwa sababu ya fashini, mitindo na utamaduni wao. Kuongezeka kwake miongoni mwa watu kumesababisha kuongezeka kwa tasnia ya mitindo duniani. Hii inaonyesha kwamba tamthilia za Kikorea za kila siku zimeweza kufikia viwango vya juu. 

Mwandishi mmoja kwa kawaida huongoza filamu za Kikorea, ambazo mara nyingi huandikwa na mwandishi mmoja wa skrini pia. Hii mara nyingi hupelekea kila filamu kuwa na mitindo tofauti ya uelekezaji na mazungumzo. Hii inatofautiana na mfululizo wa televisheni za Kimarekani, ambazo zinaweza kutegemea wakurugenzi na waandishi wengi kufanya kazi pamoja. [2]

Muda wa saa 1:00 jioni hadi 3:00 usiku kwa kawaida umetengwa kwa ajili ya drama za kila siku, ambazo hufanyika kila usiku kutoka Jumatatu hadi Ijumaa. Kuna filamu za wikendi muda wa saa 4:00-6:00 usiku pia.

Msuko wa hadithi na maudhui

hariri

Filamu za Kikorea zina aina nyingi tofauti kama drama za mapigano, drama za kihistoria, drama za shule, tamthilia za kimatibabu, filamu za kisheria au hata za ucheshi na za kutisha. Ingawa tamthilia nyingi huwa na mambo ya kimapenzi na mandhari ya kina ya hisia, baadhi pia zinaweza kuwa na mkasa au kipande cha mandhari ya maisha. Kuna mitindo mbalimbali.

Mada kuu za drama za televisheni za Kikorea ni urafiki, maadili ya kifamilia, upendo, na ubinafsi. Hata hivyo kuna mwelekeo unaoibuka miongoni mwa filamu za Kikorea kuonyesha masuala yanayoendelea ya kijamii ya jamii za Korea, kama unyanyapaa wa ugonjwa wa akili, ukosefu wa usawa wa kijinsia, kujiua, matabaka, uonevu, kamera za kijasusi, rushwa, chuki kwa wapenzi watu wa jinsia moja au ubaguzi wa kimbari. [3]

Muziki

hariri

Muziki una umuhimu mkubwa katika filamu za Kikorea. Original Soundtrack, inayofupishwa kama OST, hutungwa kwa kila tamthiliya, na tofauti na tamthiliya za Kimarekani, mashabiki hupenda kununua albamu ya sauti ya filamu kwa kawaida. Mtindo huu ulianza katika mwaka wa 1990, wakati watengenezaji wa muziki walipobadili ala za muziki kwa nyimbo zilizoimbwa na waimbaji maarufu wa K-pop.

Filamu zinazopendwa zaidi za K-drama, “Desendant of the Sun,” “My Love from the Star,” “Boys Over Flowers,” “Extraordinary Attorney Woo,” “The Glory,” “Sky Castle,” “Crash Landing on You,” na “Goblin.”

Marejeo

hariri
  1. "외국에서도 우리나라 드라마가 인기래요". terms.naver.com (kwa Kikorea). Iliwekwa mnamo 2023-04-23.
  2. "Digital Chosunilbo (English Edition) : Daily News in English About Korea". web.archive.org. 2007-01-10. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-01-10. Iliwekwa mnamo 2023-04-23.
  3. https://namu.wiki/w/한국%20드라마