Korea ya Kusini (jina rasmi: Jamhuri ya Korea) ni nchi ya Asia ya Mashariki iliyopo kusini mwa rasi ya Korea.

Korea Kusini
Ramani ya Korea ya Kusini

Upande wa kaskazini imepakana na Korea ya Kaskazini. Korea zote mbili zilikuwa nchi moja hadi mwaka 1945 chini ya utawala wa kikoloni wa Japani.

Ng'ambo ya bahari iko Uchina upande wa magharibi na Japani upande wa kusini-mashariki.

Mji mkuu, pia mji mkubwa, ni Seoul ambako karibu nusu ya wakazi wote huishi ama mjini ama katika mazingira yake. Seoul ni kati ya miji muhimu ya biashara na uchumi kimataifa.

Historia hariri

Utamaduni wa Korea ni kati ya zile za kale zaidi duniani.

Tangu maungano ya kitaifa ya Korea yote mwaka 668 KK ilikuwa nchi moja hadi mwaka 1910 ilipofanywa koloni la Japani.

Uhuru baada ya mwaka 1945 ulifuatwa na mgawanyiko wa nchi na kuundwa kwa Korea Kusini.

Awali ilikuwa nchi maskini yenye uchumi wa kilimo, lakini iliendelea kuwa nchi ya viwanda iliyofaulu kusogea mbele na kujenga demokrasia imara.

Siku hizi imekuwa moja ya nchi tajiri ya Asiaː ina nafasi ya 13 duniani kati ya mataifa matajiri. Iko kati ya nchi kumi duniani zinazouza bidhaa nyingi nje.

Hali ya maisha ni ya juu na viwanda vyake vinatengeneza bidhaa za kisasa kabisa kama motokaa, meli, mashine, vifaa vya kompyuta na nyinginezo.

Miji hariri

Mikoa hariri

Kuna mikoa tisa nchini Korea Kusini, zikiwemo:

Watu hariri

Wakazi karibu wote (99 %) ni Wakorea asili. Wachina ni 1.8 %, lakini wengi wao wana asili ya Korea.

Idadi ya watu inaelekea kupungua kutokana na uzazi kuwa wa nadra mno (watoto 9 kwa watu 1,000ǃ).

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kikorea.

Dini hariri

Kiasili watu wa Korea walifuata dini ya jadi iliyoheshimu mapepo mbalimbali na kutoa sadaka kama njia za kuyapatanisha.

Tangu karne ya 4 Ubuddha uliingia kutoka China ukawa dini rasmi.

Ukonfusio ulifuata tangu karne ya 13.

Ukristo ulingia pia kutoka China ukaanza kukua zaidi tangu karne ya 19.

Siku hizi takriban nusu ya Wakorea wa kusini wasema hawana dini. Sehemu kubwa wanakadiriwa kuwa wafuasi wa Konfusio lakini hawajiiti "wanadini".

Ukristo ni kundi kubwa la kidini ukiwa na 29 % za Wakorea wa Kusini, wakiwemo Waprotestanti (18.3 %) na Wakatoliki (10.9 %). Wabuddha ni kama 22.8 %. Kuna pia wafuasi wachache wa dini nyingine mbalimbali.

Tazama pia hariri

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.