Flortaucipir (18F)

Flortaucipir (18 F), inauzwa kwa jina la chapa Tauvid, ni ajenti ya uchunguzi wa mionzi inayotumika katika upigaji picha wa kitomografia wa positron emission (PET) wa ubongo katika Alzeima (Alzheimer).[1] Sio muhimu kwa ugonjwa sugu wa ubongo unaoendelea unaoharibika mara nyingi unaohusishwa na majeraha ya kichwa ya mara kwa mara (chronic traumatic encephalopathy).[1] Dawa hii inatolewa kwa njia ya sindano kwenye mshipa.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maumivu ya kichwa, maumivu ya mahali pa sindano, na kuongezeka kwa shinikizo la damu.[1] Madhara yake mengine ni pamoja na mfiduo wa mionzi.[1] Dawa hii inafanya kazi kwa kujifunga kwenye mahali pa ubongo panapohusishwa na kujikunja kubaya kwa protini ya tau.

Flortaucipir (18 F) iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2020.[1] Haijaidhinishwa kutumika Ulaya au Uingereza kufikia mwaka wa 2022.[2]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Tauvid- flortaucipir f-18 injection, solution". DailyMed. 22 Julai 2020. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Mei 2022. Iliwekwa mnamo 28 Mei 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Flortaucipir F18". SPS - Specialist Pharmacy Service. 28 Novemba 2020. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 Januari 2022. Iliwekwa mnamo 4 Novemba 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Flortaucipir (18F) kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.