Frank Martin ni uhusika uliochezwa na Jason Statham, hasa katika mfululizo wa filamu za The Transporter. Martin amecheza kama dereva wa kulipwa-kujitegemea, anapatika kwa jamii ya wateja matajiri au hata wale wa uhalifu, ambaye anaishi hasa kwa kupata fedha kutoka katika shughuli za usafirishaji wa vitu.

Frank Martin

Jason Statham kama Frank Martin katika The Transporter. Mwigizaji filamu wa Kitaiwani Shu Qi kacheza kama Lai Kwai.
Mwonekano wa kwanza The Transporter
Maelezo
Majina mengine Driver
The Transporter
Jinsia Male
Umri Haujulikani
Tarehe ya kuzaliwa Haijulikani
Kazi yake Usafirishaji na Mpanda baiskeli

Jason Statham yeye mwenyewe ni mhitimu wa mafunzo ya martial arts, inamruhusu kufanya michezo ya hatari ikiwa ni pamoja na nyusika za Frank Martin. Hii imeifanya filamu kuwa na vipande vya kupiga visivyokatwa katika na alama za ukweli zilizoongozwa na Cory Yuen.

Historia ya uhusika

hariri

Martin anacheza kama opereta wa zamani wa kikosi maalumu ambapo alikuwa kiongozi wa kikosi cha utafiti na maangamizi. Historia yake ya kijeshi inaonesha kwamba alisha-zuru katika operesheni kadhaa ikiwa ni pamoja na Lebanon, Syria na Sudan. Amejizuru katika kazi hii ni baada ya kukasirishwa na moja ya wakubwa zake kwa kudharau kazi yake na kuona hana analolifanya, lakini kwa ufupi ni kwamba amechoshwa kuona juhudi zake za dhati zinageuka kuwa si kitu na watu walewale wanaomlipa kufanya kazi, halafu kutumia maarifa yake kufanyia shughuli za kishenzi.

Nchi na asili ya Martin bado haieleweki - mbali na kazi, Statham ameathiriwa na lafudhi za "Kiatlantiki", anakichanganya mwenyewe na lahaja ya Kiingereza cha Mashariki na lafudhi ya Kiingereza cha Kimarekani, huenda akawa labda Mwigingereza au Mwamerika, lakini ni mtu ambaye anatumia muda wake mwingi kuishi katika nchi nyingine.

Katika The Transporter, ameonekana kupata Nyota ya Shaba.

Inawezekana kwamba awali wakati akiwa jeshini, Martin alicheza kama mtaalamu wa milipuko, upelelezi, mkali wa kupiga mkono kwa mkono, mpishi na mwendeshaji gari kwa kuhepahepa. Akisisitiza kwamba yeye ni dereva mhitimu, anaweza kufanya maujanja na nguvu za kudhibiti chombo pindi aendeshapo gari lake. Martin mara nyingi hujiingiza kwenye ngumi za mkono kwa mkono, uwezo wa kubuni na kutumia silahi zisizo za kawaida dhidi ya mpinzani. Martin pia ni mhitimu wa kupiga risasi haraka sana.

Sheria

hariri

Martin hufanya shughuli zake kwa sheria kadhaa,[1] ambazo hataki kuzivunja katakata, na kutarajia wateja wake zake kuzitekeleza kwa njia ya kuonana au kwa simu. Sheria zake ni pamoja na:

  1. "The deal is the deal" = Makubaliano ni makubaliano
  2. "No names" = Hakuna kutaja majina
  3. "Never open the package" = Hakuna kufungua mzigo
  4. "Never Make A Promise You Can't Keep" = Usiweke Ahadi Usiyoweza-Kuitimiza

Wakati wa mwanzoni kabisa mwa sheria hizi zimeonekana kutokuwa na umuhimu, umuhimu wake ulionekana pale Frank alipokodishwa kama dereva mtoroshaji, na mwanachama mwingine wa ujambazi akaongezeka. Akamweleza mkubwa wa majambazi kwamba idadi kamili ya abiria ilishakubaliwa kwa maana hiyo Martin anaweza kurekebisha mpango mzima, kiongozi wa majambazi akalazimika kumwua jambazi mmoja ili kuweka idadi kamili ya abiria, au achukue hatua kwa kuvunja sheria. Martin ameonekana akivunja sheria zake mwenyewe kuhusu kutofungua mzigo katikati mwa filamu ya The Transporter.

Sheria nyingine zimedokezwa na tabia ya Frank katika mfululizo yake ya kazi. Sheri hizo ni pamoja na, lakini hazina kikomo kuwa ndiyo mwisho, la:

  1. "Always buckle up" = Daima funga mkanda
  2. "Just say no to drugs" = Pinga madawa ya kulevya
  3. "Never have friends who can speak English" = Kamwe -siwe na rafiki asiyeweza kuonge Kiingereza
  4. "Never hit a woman, even if she's messing around with your car keys for a good five minutes" = Usimpige mwanamke, hata kama anavuruga funguo za gari lako hata kwa dakika tano
  5. "50% discount if not delivered in specified time" = Punguzo la 50% iwapo mzigo utafika kwa muda usio-mwafaka
  6. "Drive your own car, unless the other guy's are faster" = Endesha gari lako mwenyewe, isipokuwa la vijana wengine ambao wanaenda kwa fujo

Sheria za gari:

  1. "Respect a man's car, and the man will respect you" = Heshimu gari la mtu, na huyo mtu atakuheshimu
  2. "Greet the Man" = Salimia mtu
  3. "Seat belt" = Funga mkanda

Mwonekano

hariri

Martin hujali mpangilio wa sare, kwa kuvaa suti nyeusi, shati leupe, na tai nyeusi. Martin pia hujali suala la muda.

Magari

hariri

Martin anaonekana kupenda magari ya milango minne, kwa kutumia BMW 735i E38 na Mercedes-Benz W140 katika The Transporter, 2004 Audi A8 6.0 W12 katika Transporter 2 na 2008 Audi A8 6.0 W12 kwenye Transporter 3. Hata hivyo, wakati utengeneza wa moja ya sehemu ya filamu ya Transporter 2, aliindesha Lamborghini Murcielago Roadster.

Marejeo

hariri

Viungo vya Nje

hariri