Syria au Siria (kwa Kiarabu: سوريا au سورية ) ni nchi ya Mashariki ya Kati au Asia ya Magharibi.

الجمهورية العربية السورية
Al-Jumhūriyyah al-ʿArabiyyah as-Sūriyyah

Jamhuri ya Kiarabu ya Syria
Bendera ya Syria (Shamu) Nembo ya Syria (Shamu)
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: --
Wimbo wa taifa: Homat el Diyar
"Walinzi wa nchi"
Lokeshen ya Syria (Shamu)
Mji mkuu Dameski
33°30′ N 36°18′ E
Mji mkubwa nchini Dameski
Lugha rasmi Kiarabu
Serikali Jamhuri
--
Muhammad Naji al-Otari
Uhuru
Ilitangazwa (1)
Ilitangazwa (2)
Ilitambuliwa

Septemba 19361
1 Januari 1944
17 Aprili 1946
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
185,180 km² (ya 89)
1.1
Idadi ya watu
 - Julai 2014 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
17,951,639 [1] (ya 54)
118.3/km² (101)
Fedha Lira ya Shamu (SYP)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
EET (UTC+2)
EEST (UTC+3)
Intaneti TLD .sy
Kodi ya simu +963

-

1 Mkataba kati ya Ufaransa na Syria ya 1936 haikutambuliwa awali na Ufaransa.


Ramani ya Syria

Imepakana na Lebanon, Israel, Yordani, Iraq na Uturuki.

Kuna pwani kwenye bahari ya Mediteranea.

Nchi inatajwa pia kwa jina la "Shamu" katika maandiko ya Kiswahili, ingawa neno hili lamaanisha zaidi eneo la kihistoria ambalo lilikuwa kubwa kuliko Syria ya leo.

Historia

hariri
 
Wanawake wa Syria, mwaka 1683.

Nchi ilikaliwa na watu tangu milenia nyingi. Ilipata kuwa chini ya utawala wa Misri hadi mnamo mwaka 1100 KK.

Ufalme wa Aramu

hariri

Tangu mwaka 1000 KK hivyo kulikuwa na ufalme wa Aramu unaotajwa mara nyingi katika Biblia pia, ukiwa na makao makuu mjini Dameski. Baada ya kushindana mara nyingi na Israeli ulikwisha katika vita dhidi ya Assyria mwaka 732 KK.

Utawala wa Babeli, Uajemi, Wagiriki na Roma

hariri

Assyria ilishindwa na Nebukadreza II wa Babeli na Syria ikawa sehemu ya milki ya pili ya Babeli tangu 572 KK.

Mwaka 538 KK, Uajemi ilipochukua nafasi ya Babeli, Dameski ikawa mji mkuu wa jimbo la Syria.

Kufika kwa Aleksanda Mkuu tangu 333 KK kulibadilisha siasa ya Mashariki ya Kati na Syria ikawa sehemu ya ustaarabu wa Kigiriki.

Tangu mwaka 64 KK Dola la Roma likaingia Shamu. Dameski ikawa mji mkuu wa jimbo la Kiroma likakua na kustawi. Barabara na majengo ya nyakati zile za Waroma yanaonekana hadi leo, kwa mfano barabara ya decumanus, ambayo imetajwa katika Biblia ya Kikristo kama "barabara iliyonyoka" au "barabara iitwayo Nyofu" (Mdo 9:11).

 
Maziara ya kichwa cha Yohane Mbatizaji ndani ya msikiti wa Muawiya mjini Damasko yanatembelewa na Waislamu na Wakristo vilevile.

Waarabu na Waosmani

hariri

Syria ilivamiwa na jeshi la Waarabu Waislamu chini ya khalifa Umar I mwaka 636 B.K..

Baada ya ushindi wa Muawiyya mwaka 661 juu ya Hussain ibn Ali alichukua cheo cha khalifa akikaa Dameski. Hivyo mji ukawa mji mkuu wa milki ya Wamuawiya iliyotawala kutoka Hispania hadi milango ya China.

Khalifa wa mwisho wa Wamuawiya Marwan II alihamisha makao yake kwenda Haran katika Mesopotamia ya kaskazini. Marwan alishindwa baadaye na Abu al-`Abbās `Abdu'llāh as-Saffāh aliyeanzisha utawala wa makhalifa Waabbasi na kupeleka mji mkuu Baghdad.

Salah-ad-Din aliweka tena nchi chini ya utawala wa Misri hadi 1516, ambapo Milki ya Waturuki Waosmani ulianza kutawala ukaendelea hadi 1918, ila baina ya miaka 1832 na 1840 walipotawala Wamisri.

Wakati wa utawala wa Waosmani, Wayahudi na Wakristo wa Dameski waliweza kuendelea na dini zao wakiwa dhimmi (watu wasio Waislamu na waliolazimisha kulipa kodi kubwa kuliko ya Waislamu).

Mwanzo wa karne ya 20, wazo la utaifa wa Kiarabu lilianza Dameski kwa sababu ya sheria kutoka Istanbul ambazo zilitumiwa zibadilishe Dameski iwe “mji wa Kituruki” zaidi. Utekelezaji wa watu wenye elimu mwaka 1915 na mwaka 1916 ulikuza hilo wazo la utaifa wa Kiarabu. Lakini Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilivunja milki ya Waosmani ikaleta utawala wa Ufaransa katika Syria.

Baada ya vita vikuu vya kwanza

hariri

Mwaka 1918, mapinduzi ya Waarabu yalianza nchini Syria na baada ya muda mfupi, Waosmani waliondoka Syria na Waingereza walichukua nchi. Faisal ibn Hussein alikuwa mfalme mpya wa Syria. Mwaka 1920, serikali iliandika katiba mpya ya kidemokrasia. Lakini, mwaka huohuo Mkutano wa Versailles aliutolea Ufaransa nchi ya Syria. Hivyo kati ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia na uhuru ilikuwa nchi lindwa chini ya Ufaransa kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa[2].

Mwaka 1925, mapinduzi mapya ambayo yalianzishwa na Hauran (eneo la mashamba kusini mwa nchi) yalifika Dameski. Wasyria walitaka uhuru wao. Lakini, Ufaransa ulitupa mabomu Dameski na waliacha mapinduzi.

Syria ya kisasa imepata kuwa nchi ya kujitawala kwa hatua mbalimbali tangu mwaka 1936 hadi kukamilisha uhuru wake baada ya Vita vikuu vya pili vya dunia mwaka 1946.[2]

Syria imetawaliwa na chama cha Baath tangu mwaka 1963; tangu mwaka 2000 rais ni Bashar al-Assad, aliyemrithi baba yake Hafez al-Assad aliyetawala kuanzia mwaka 1970.

Syria ilishiriki katika vita vya Waarabu dhidi ya Israel. Hivyo sehemu ya Mkoa wa Qunaytrah imekaliwa na Israel tangu mwaka 1967.

Tangu Machi 2011 nchi imeingia vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoua watu zaidi ya 100,000 kufikia Septemba 2013 na kufanya wananchi milioni 9.5 kukimbia nyumba zao. Kati yao milioni 4 wako nje ya nchi. Wakati fulani nusu ya nchi ilitawaliwa na DAESH.

Tarehe 8 Desemba 2024 wapinzani, baada ya Aleppo, waliteka Damasko, hivi kwamba rais Assad alilazimika kukimbia nchi.

Syria kiutawala imegawiwa katikaa mikoa (muhafazat) 14:

Lugha ya kitaifa ni Kiarabu. Waarabu ni 74% za wakazi.

Kuna pia maeneo yenye Wakurdi (9%), Waturuki (3-5%), Waaramu (2%), Waarmenia na wengineo ambao wanaendelea kutumia lugha zao.

Wasyria walio wengi ni Waislamu (74%), hasa Wasunni lakini kuna pia wafuasi wengi kidogo wa aina ya Washia wanaoitwa "Waalawi" n.k. (13%).

10% za wakazi ni Wakristo, wakiwemo kwanza Waorthodoksi wa Mashariki, halafu Waorthodoksi (35.7% za Wakristo wote) na Wakatoliki (26.2%).

3% ni Wadruzi.

Wayahudi wamekuwa wachache sana kutokana na ugomvi kati ya Waarabu na Israel.

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. "The World Factbook". CIA. Retrieved 2014-07-24.
  2. 2.0 2.1 "Report of the Commission Entrusted by the Council with the Study of the Frontier between Syria and Iraq". World Digital Library. 1932. Iliwekwa mnamo 2013-07-11.

Viungo vya nje

hariri
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Syria kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.