Frodo Baggins

Frodo Baggins ni mhusika katika vitabu vya bunilizi ya kinjozi vilivyoandikwa na J.R.R. Tolkien.

Frodo by Mark Ferrari

Kwa mbari, Frodo ni mhobiti. Hadithi yake hasa yasimuliwa katika Bwana wa Mapete. Amerithi Pete Kuu kutoka kwa mjomba wake, Bilbo Baggins, akasafiri kutoka nchi ya Shire, yaani nyumbani kwake, hadi nchi ya Mordor ili kuteketeza pete na kumshinda Bwana mwovu Sauron.