Gifted Hands, The Ben Carson Story

Gifted Hands, The Ben Carson Story ni hadithi ya kweli inayohusu maisha ya Daktari mtaalamu wa Nyurolojia Ben Carson Katika kitabu hiki, Carson anaelezea historia yake kuanzia alivyokuwa mtoto katika eneo la Detroit hadi wakati akiwa mkurugenzi wa idara ya watoto ya Nyurolojia katika Hospitali ya Johns Hopkins akiwa na umri wa miaka 33. Kitabu hiki kilichapishwa na kutoka mwaka 1996 kikiwa kimetengenezwa na mwandishi maarufu Cecil Murphy.

Mandhari ya Kitabu

hariri

Kitabu cha Gifted Hands, kimendikwa kwa kufuata eneo halisi alilokuwa akiishi Ben Carson na kukulia hapo, eneo la Detroit nchini Marekani na badae kwenda kusoma katika chuo kiku cha Yale katika masomo yake ya udaktari

Sehemu ya Kwanza

hariri

Katika sehemu ya kwanza ya kitabu hiki, inaeleza jinsi mama yake Ben anayeitwa Sonya Carson akiwaelezea watoto wake kuwa baba yao hatarudi nyumbani,na hali ya kutokuwa na fedha katika familia yao. Ben anajari kusisitiza mama yake amsisitize baba yao arudi nyumbani bila mafanikio, na hadi mwisho wa sehemu hiyo,mama yake Ben anajaribu kuwaonesha watoto wake kuwa hakuna njia itakayomfanya baba yao arudi nyumbai.

Sehemu ya Pili

hariri

Katika sehemu hii, Sonya Carson ambaye ni mama yeke Ben na kaka yake Curtis, anakasirika kutokana na Curtis kuhgamishiwa katika shule ya ufundi. Mama yake Ben anazidiwa na kupata ugonjwa wa akili na hivyo anawaaga watoto wake kuwa anakwenda mbali kwa muda wa siku chache na anatumia nafasi hiyo kuhudhuria matibabu ya ugonjwa wa akili.

Sehemu ya tatu

hariri

Curtis na Ben pamoja na mama yao wamehamia katika eneo ambalo li la hali ya chini zaidi, mama yao akiendelea kufanya kazi katika sehemu mbili au zaidi. Akiwa na miaka minane tu, Ben anapenda moja ya mifano iliyoliyoku waikitolewa na mchungaji katika kanisa lao la Kisabato, na baadae wakati wa kutoka kanisani, Ben anamwambia mama yake kuwa angependa kuwa daktari pindi atakapokuwa mkubwa, na mama yake anakubali.Lakini bado Ben alikuwa anafanya vibaya darasani akipata alama sifuri katika masomo mbalimbali.

Sehemu ya tatu

hariri

Ben na kaka yake wanaendelea kupatwa na matatizo ya kubaguliwa katika maeneo mengi, lakini kwa wakati huu, Ben anafanya vizuri kidogo katika somo la Hesabu japo mama yake bado anaamini kuwa angeweza kufanya vizuri zaidi. Wanajaribu kumficha mama yao juu ya mambo mbalimbali ya kibaguzi wanayokumbana na yo ili kumkinga asiumie na matati zaidi.

Sehemu ya nne

hariri

Akiwa anefanya vizuri sasa katika masomo yake, Ben anaendelea kukabiliwa na mambo ya kibaguzi katika shule ya Hunter Junior High.Na ndio katika wakati huu hasa,,Ben natambua umuhimu wa Mungu katika maisha yake. Katika sehemu ianyofuatia yaani sehemu ya tano,Ben ana kabiliwa na hasira ya ajabu,anajari hata kumuua rafiki yake anaitwa Bob na kisu na ndipo Ben anapogeuka na kuanza kuani uwepo na msaada wa Mungu katika maisha yake.

Kuanza kupenda Udaktari

hariri

Ben alionesha dalili za kuwa daktari akiwa bado mdogo sana, kutokana na kumwona kaka yake akiwa na nguo za jeshi la ROTC Ben alivutiwa na kuamua pia kujiunga na jeshi, alifanya vizuri sana akiwa huko na kupata nafasi mbalimbali za uongoza kiasi cha kumpita kaka yake. Baadae aliacha jeshi na kuanza kujifunza muziki. lakini hadi wakati huu, bado aliendelea kupenda kuwa daktari.

Kuelekea kutimiza ndoto

hariri

Kuchagua Chuo

hariri

Wakati wa kuchagua chuo ulipofika Ben alikumbana na mtihani mwingine, akiwa na dola kumi ambayo ndio kiingilio halisi cha fomu ya kujiunga, Ben alitaka kuchagua kati ya chuo cha Yake na chuo kikuu cha Harvard. Baadae aliamua kuchagua na hatimaye kujiunga na chuo kikuu cha Yale ambapo huko alipata vikwazo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushindwa kuelewa baadhi ya masomo hususani somo la Kemia na kupata muujiza wa kuota mtihani. Akiwa chuoni, Ben anakutana na msichina aniyeitwa Candy, ambaye baadae ndiye anakuja kuwa mke wake.Baadae Ben anakuwa daktari na kuanza kazi katika Hospitali ya Johns Hopkins.

Akiwa Kazini

hariri

Akiwa kazini katika hospitali ya Johns hopikins, Dr Ben anafanya upasuaji wa hali ya juu, huku siku za mwanzo akikabiliwa na hali ya ubaguzi kutokana na yeyey kuwa mwenye asili ya Afrika. Lakini Dr Ben anafanikiwa kufanya upasuaji ambao kwa hakika ulionekana maajabu, hususani alipoongoza timu ya madaktari waliotenganisha mapacha wawili waliokuwa wameungana katika eneo la kichwani na watoto wote kuweza kuishi baada ya Upasuaji huo.

Familia yake

hariri

Akiwa na watoto wawili, na mke wake Candy Ben anatoa mwanga kwa watoto wadogo hususani wanookuwa na kuwa na vipaji maalumu, kugundua vipaji vyao na kuvifanyia kazi ili kuweza kufikia malengo yao. Ben na Candy wanapanga kuanzisha taasisi itakayowasaidia watoto wadogo wenye vipaji likini hawana uwezo wa kusoma. Anaendelea katika kitabu cha "Think Big"

Mrejeo

hariri
  1. ISBN 0-310-21469-6