Mikono Yenye Vipawa: Hadithi Ya Ben Carson

Mikono Yenye Vipawa: Hadithi Ya Ben Carson ni filamu ya mwaka wa 2009 iliyoandaliwa na Thomas Carter na kuigizwa na Cuba Gooding Jr na Kimberly Elise. Inazingatia hadithi ya maisha ya daktari maarufu wa upasuaji, Ben Carson, kati ya miaka ya 1961 na 1987. Filamu yenyewe imeandaliwa na Johnson na Johnson Spotlight Presentation na ilionyeshwa kwenye stesheni ya TNT tarehe Jumamosi 7 Februari 2009. Jina la filamu hii ilikuwa imetumika hapo awali 1992 kwa filamu fupi kuhusu Ben Carson iliyotolewa na Zondervan,ingawaje filamu hizi ni tofauti.

Filamu kuhusu Ben Carson

Hadithi yenyeweEdit

Ben Carson, Cuba Gooding, anaanza maisha akiwa katika hali ya taabu nyingi: yeye akiwa mtoto wa asili ya Kiafrika huko Marekani,hana baba na masomo yamemshinda shuleni.Inaanza akiwa akila vyakula kama vibanzi akitazama runinga na anahitaji miwani. Mama yake aliyeacha shule akiwa daraja la tatu,anaanza kufanya maamuzi kwa aljili yake kwa kuwa anaona mienendo yake Ben ni mbovu. Wana wake wawili,Ben na Curtis, walipohitaji kujua hesabu ya kuzidisha aliwafanya waape kuwa watasoma yeye akiwa ameenda ukaguzi katika taasisi ya waliorukwa na akili.

Mama yao anapoona kizuizi cha ufanisi wa wana wake ni runinga anawaagiza wasome vitabu viwili kila wiki kutoka maktaba na kuandika ripoti kuvihusu. Anawapeleka,pia, kwa shule bora zaidi.

Wakati uo huo, Ben anaanza kunawiri kimaisha na kiakili. Yeye anapata miwani alizohitaji. Yeye anajifunza hesabu ya kuzidisha. Yeye anaanza kutafiti ulimwengu wa vitabu, na anaendelea kukua ndani yake. Ben anaanza pia kuwa na hasira nyingi,hasira huu ungemharibia utoto wake isipokuwa muujiza uliomfanyikia.

Baada ya kukaribia kumwua mtu kwa ghadhabu zake,aligundua kuwa ameshikwa mateka na hasira hizo na alihitaji kufanya marekebisho haraka. Yeye anaenda chumbani mwake na kumlilia Mungu na kuomba kwamba anaweza kumkomboa kutoka hasira.

Yeye anaongoza chuoni katika darasa lake la daraja la nane. Anaendelea kufaulu hadi kuwa nambari tatu akiwa shule ya upili. Kwa jitihada na njaa ya ufanisi, anapata udhamini unaomwezesha kuenda chuo kikuu.Anapita mtihani wa somo la udaktari na hiyo inamwezesha kuenda shule ya kufunza madaktari na nesi.

Carson anapata maisha magumu akiishi na madaktari na wanafunzi wenzake akifanya kazi katika Hospitali ya Johns Hopkins.Akiwa huku ndiko alikofanya upasuaji kama mkazi bilia kuhudhuriwa na msimamizi akihatarisha kazi yake ya udaktari ili kuokoa maisha ya mgonjwa.

Ben Carson anaigwa kama daktari wa upasuaji mwenye kipaji na hivyo basi kuipa kitabu chake na filamu,Mikono Yenye Vipawa(yaani Gifted Hands).

WaigizajiEdit

Dhima Mwigizaji Vidokezo
Benjamin "Bennie" Carson Cuba Gooding Jr. Dhima muhimu kabisa katika filamu.
Sonya Carson Kimberly Elise Mama Ben
Candy Carson Aunjanue Ellis Mke wa Ben
Bennie akiwa kijana wa shule ya upili Gus Hoffman Ben Carson akiwa kijana
Bennie Jaishon Fisher Ben Carson akiwa mtoto

IlivyopokewaEdit

Wakosoaji wameipa filamu hii jumla ya kitaalam wa 63/100 katika tovuti ya Metacritic.com. The Orlando Sentinel inasema, "Filamu hii ni bora kwa nchi iliyopewa changamoto na rais wake mpya kufanya vizuri."

Viungo vya njeEdit