Giovanna Epis
Giovanna Epis (alizaliwa 11 Oktoba 1988) ni mwanariadha wa mbio za umbali mrefu kutoka nchi ya Italia, alishindana kwenye michuano ya IAAF World Half Marathon ya mwaka 2018[1]. Alishinda medali ya shaba akiwa na timu ya Italia kwenye michuano ya 2019 European 10,000m Cup jijini London. Mwaka 2019, alishindana kwenye marathoni ya wanawake kwenye michuano ya 2019 World Athletics Championships yaliyofanyika Doha, Qatar[2]. Hakufanikiwa kumaliza mbio hizo. Alishiriki marathoni kwenye Olimpiki ya majira ya joto mwaka 2020[3]
Marejeo
hariri- ↑ "Giovanna Epis (c.s. Carabinieri Sez. Atletica)". www.fidal.it (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-09-27.
- ↑ "Wayback Machine" (PDF). web.archive.org. 2019-09-28. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2019-09-28. Iliwekwa mnamo 2021-09-27.
- ↑ "Athletics EPIS Giovanna - Tokyo 2020 Olympics". olympics.com (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-09-27. Iliwekwa mnamo 2021-09-27.