Glenn Ford (Mei 1, 1916 - Agosti 30, 2006) alikuwa mwigizaji maarufu wa filamu kutoka Canada-Marekani. Enzi yake alitamba sana kwa kazi zake katika sinema za Hollywood. Zaidi ilikuwa kati ya miaka ya 1940 na 1970. Alizaliwa huko Quebec, Canada na jina lake kamili lilikuwa Gwyllyn Samuel Newton Ford. Glenn Ford alihamia Marekani akiwa mtoto. Alianza uigizaji katika michezo ya jukwaani kabla ya kuingia kwenye filamu.

Glenn Ford - 1955.
Marguerite Chapman-Glenn Ford katika filamu ya Destroyer.

Baadhi ya filamu maarufu za Glenn Ford ni Gilda (1946), ambapo alicheza kama Johnny Farrell, The Big Heat (1953) kama polisi aliyeazimia kulipiza kisasi, Blackboard Jungle (1955) kama mwalimu anayekabiliana na changamoto za kufundisha kwenye shule yenye wanafunzi wenye tabia mbaya, na 3:10 to Yuma (1957), ambapo aliigiza kama mhalifu.

Glenn Ford alifariki mnamo Agosti 30, 2006, akiwa na umri wa miaka 90. Ameacha urithi wa filamu nyingi za kuvutia huku akichukuliwa kama mmoja wa waigizaji wa heshima katika historia ya Hollywood.

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


  Makala hii ni sehemu ya mradi wa kuboresha Wikipedia na Wikamusi ya Kiswahili. Unaweza kusaidia kuihariri na kuongeza habari.