Gloria Young
Gloria Young (alizaliwa tarehe 4 Februari 1967) ni mwigizaji wa kike wa Nigeria aliyeshiriki Zaidi ya filamu 70 na alishinda tuzo ya filamu ya City People Movie Award. [1] [2]
Maisha na elimu
haririYoung alizaliwa katika jimbo la Abia inayopatikana kusini mashariki mwa Nigeria. Alipata elimu ya msingi katika shule ya Fountain iliyopo Surulere, jimbo la Lagos (jimbo). Alihitimu shule ya upili ya wasichana Methodist iliyopo Yaba Lagos. Young alipata shahada ya sayansi nchini Marekani. [3] [4][5]
Kazi
haririYoung alianza kazi kama mwandishi wa habari[6] Kisha akajihusisha na burudani na kuwa mtumbuizaji katika tamasha la Charly Boy. Kazi yake ya uigizaji ilianza mwaka 1994 alipochukua uhusika katika filamu inayoitwa “Glamour Girls”. [7] Na hatimaye filamu hiyo ilifanikiwa kuwa mradi wenye mafanikio. Young alicheza filamu ya Glamour Girls kama Doris. Filamu hiyo ilihusisha waigizaji maarufu wa Nigeria kama vile Liz Benson, Eucharia Anunobi, Dolly Unachukwu, Keppy Ekpenyong, Sola Fosudo, Ngozi Ezeonu, na Sandra Achums. [8][9][10][11]
Filamu zake
hariri- Flee
- Passionate Appeal
- The Soul That Sinneth
- Wanted At All Cost
- Back To Life
- The Return
- Deadly Affair
- Glamour Girls
Tuzo
haririMwaka | Tuzo! Kipengele | Matokeo | ||
---|---|---|---|---|
2018 | City People Entertainment Awards | Movie Couple of the Year | mshindi | [2] |
Marejeo
hariri- ↑ "I didn't sleep with anyone to be movie star – Gloria Young". The Sun Nigeria (kwa American English). 2018-08-11. Iliwekwa mnamo 2019-12-04.
- ↑ 2.0 2.1 People, City (2018-09-24). "Winners Emerge @ 2018 City People Movie Awards". City People Magazine (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-10-10.
- ↑ "Gloria Young". Africa Magic - Gloria Young (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-02.
- ↑ Published. "Gloria Anozie-Young, others light up MUSON Festival". Punch Newspapers (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-12-02.
- ↑ "'Nollywood has many rivers to cross', Gloria Young | Encomium Magazine" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-12-02.
- ↑ "Actress Gloria Young recalls her days as struggling journalist". The Nation Newspaper (kwa American English). 2018-02-23. Iliwekwa mnamo 2019-12-02.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". guardian.ng. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-12-02. Iliwekwa mnamo 2019-12-02.
- ↑ "I've been having nightmares about Ibinabo — Gloria Anozie-Young". Vanguard News (kwa American English). 2016-03-31. Iliwekwa mnamo 2019-12-02.
- ↑ "Nollywood alternative to prostitution, robbery says Gloria Anozie-Young". Vanguard News (kwa American English). 2009-08-07. Iliwekwa mnamo 2019-12-02.
- ↑ "Gloria Anozie-Young Archives". The Guardian Nigeria News - Nigeria and World News (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-12-02.
- ↑ David, Tokunbo (2018-08-11). "I didn't sleep with anyone to be movie star – Gloria Young". The Sun Nigeria (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-12-02.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Gloria Young kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |