Dolly Unachukwu

Muigizaji wa

Dolly Unachukwu (alizaliwa tarehe 1 Novemba 1969) ni muigizaji kutoka nchini  Nigeria .[1]

Dolly Unachukwu

Dolly Unachukwu mnamo 2020
Amezaliwa Dolly Nchedo Nkem Unachukwu
1 Novemba 1969 (1969-11-01) (umri 54) Lagos, Nigeria
Kazi yake Muigizaji Mtunzi, Mtayarishaji, Muongozaji
Miaka ya kazi 1986- hadi sasa
Ndoa Emmanuel Nwokenkwo
Watoto 2, Ody Nwokenkwo (Billions CFL), Hazel Okoro

Dolly Unachukwu ni mmoja wa waanzilishi wa  Nollywood, muigizaji mwenye talanta, mwandishi, muaandaji na hivi karibuni amekuwa muongozji wa filamu, Akiwa amezaliwa  mwaka 1969 katika familia ya watoto saba , Unachukwu alianza Sanaa yake ya uigizaji akiwa na umri wa miaka 16. Mwenyeji wa Amachi katika jimbo la  Anambra, alitokea kwa mara ya kwanza katika sinema ya runingani junior drama mwaka 1985 kama katibu. Baadae mwaka huo aliigiza tena katika telenovela ya Mirror in the Sun kama  as Prisca, lakini ni uhusika wake kwenye  Fortunes ndio uliompa jina la nyumbani mwaka 1993 alipoigiza kama ‘Fadeke’ mke wa tajiri na mwanamke halisi wa Nigeria.

Mwaka 1997, Unachukwu alitoa hadithi ya maisha yake, Wildest Dream.  Kwenye filamu hiyo, anaelezea madhila ya ndoa yake ya kwanza iliyosarambatika mwaka 1994 ikimfanya kuwa mzazi mmoja/ peke yake. Mumewe huyo wa zamani alitishia kumfungulia mashtaka kwa kutumia jina lake halisi katika filamu hiyo. Unachukwu aliolewa tena mwaka 2000 na mwezi wa nane mwaka huo huo aliungana na mumewe Uingereza, ambapo waliishia kuachana uwanja wa ndege baada ya kugundua kuwa hakua mkweli kwake. Akiwa Uingereza , alipata maarifa Zaidi baaada ya kupata kibali cha udereva mwaka 2002 na mwaka uliofuata alianza shahada ya miaka mitatu ya failamu na video katika chuo cha East London, akipumzika kwa miaka miwili kwa ajili ya malezi ya mwanaye aliyezaliwa 2004, Alihitimu mwezi wa sita 2008, Unachukwu aliandaa na kuongoza filamu yake mwenyewe iliyojilikana kama The Empiremwaka  2005, wakati akiwa katika mapumziko ya chuo.

Unachukwu amesoma pia katika chuo cha Television College Jos kilichopo Jimbo la Plateau , ambapo alipata diploma ya uzalishaji wa vipindi vya runinga  mwka 1998, Pia alisomea fonetiki mwaka 1989 katika FRCN Training school Lagos na baadae kwenda chuo kikuu cha Lagos mwaka 1990 na kupata diploma (astashahada) ya sheria.

Filamu hariri

  • Mirror in the Sun (TV) 1986
  • Glamour Girls 2 1995
  • Deadly Affair II 1997
  • Deadly Passion 1997
  • Wildest Dream 1997
  • Love without Language 1998
  • Brotherhood of Darkness 1998
  • Father Moses 1999
  • Full Moon 1 & 2 1999

Marejeo hariri

  1. "Marriage Is Not My Priority - Dolly Unachukwu", Nigerian Movies & Nollywood on Naijarules.com, 2007-08-17. Retrieved on 2008-09-11. Archived from the original on 2012-09-06.