Go (kutoka Kijapani 囲碁 i-go) ni mchezo wa ubao kwa wachezaji wawili.

Ubao na kete za Go.
Mwisho wa mchezo wa Go. Kete wafungwa zimeshaondolewa. Nyeupe ina pointi 15 za eneo na Nyeusi pointi 20. Nyeupe imekamata kete 6 hivyo pointi 15+6=21, Nyeusi imekamata kete 4 hivyo ina jumla la 20+4=24, hivyo imeshinda.

Ubao wa Go

hariri

Ubao wa Go unafanywa kwa kuchora mistari ya wima 19 na mistari ya mlalo 19. Wakati mwingine, hasa kwa mchezo mfupi zaidi, hutumiwa pia ubao mdogo wa mistari 13x 13 au 9x9. Vipimo vya ubao ni baina sentimita 45 hadi 48 kwa urefu na sentimta 42 hadi 44 kwa upana.

Mchezo unafanywa kwa kutumia mikingamano ya mistari hii, si kwa kutumia miraba kati ya mistari.

Kuna aina 2 za ubao: ama ubao mbapa (jinsi ilivyo kwa sataranji au chesi) au ubao mwenye umbo la meza ndogo.

Kete za Go

hariri

Wachezaji hutumia kete ndogo, mmoja za rangi nyeusi na mwenzake za rangi nyeupe. Idadi ni kete nyeusi 181 na kete nyeupe 180, maana nyeusi inaanza. Jumla ya kete ni 361 ilhali ubao huwa na mikingamano 360 na zinatosha kufunika kila mkingamano wa ubao.

Nchini Japani wanapenda kutumia jiwe la grife kwa kete nyeusi na simbi za wakombe kwa kete nyeupe. Kuna pia kete za plastiki, za kauri au za mawe yenye rangi ya kufaa. Katika China walitumia pia mawe ya thamani.

Mchezo

hariri
 
Kama mchezaji mweupe anafaulu kuweka kete zake juu ya mkingamano zenye alama kete nyeusi zinakamatwa zinaondolewa.
 
Hapa amefaulu kukamata kete nyeusi zilizoondolewa tayari.

Mchezo huanza bila kete yoyote kwenye ubao. Mchezaji mweusi anaanza kwa kuweka kete ya kwanza juu ya mkingamano anaochagua. Mwenzake anafuata. Kila mchazaji anaweka kete moja-moja kwa zamu.

Shabaha ya mchezo ni kutawala sehemu kubwa ya ubao iwezekanavyo na kukamata kete za mpinzani. Kete inakamatwa kama inazungukwa kabisa na kete za rangi nyingine hadi kukosa nafasi ya kuongeza kete kando lake.

Kete zilizokamatwa zinaondolewa na kutunzwa kama "wafungwa". Kila "mfungwa" huhesabiwa kama pointi moja. Pointi zinahesabiwa mwishoni mwa mchezo kumgundua mshindi.

Pointi nyingine zinapatikana kwa kuhesabu mikingamano isiyo na kete katika eneo lililofungwa na kete za rangi moja.

Historia

hariri

Mchezo ulianzishwa nchini China unapojulikana kwa jina 围棋 "weiqi" tangu miaka 2000 au zaidi. Kutoka China mchezo wa Go ulisambaa hadi Korea na Japani. Leo hii kuna wachezaji kote duniani.

Go inapatikana pia kwenye intaneti kama mchezo wa online.


Marejeo

hariri

Tovuti za Nje

hariri