Kijapani (日本語 "nihon-go" au "nippon-go" ) ni lugha rasmi nchini Japani. Kinatumiwa na Wajapani karibu wote isipokuwa kundi dogo la Waainu wana lugha yao.

Idadi ya wasemaji hariri

Kwa jumla kuna wasemaji milioni 124, karibu wote wakiishi nchini Japan. Kutokana na uhamiaji kuna takriban wasemaji 420,000 nchini Marekani (zaidi ya nusu wako Hawaii) na 380,000 huko Brazil.

Uainishaji hariri

Wataalamu hawakubaliani kuhusu historia ya lugha. Lugha ya karibu ya pekee ni lugha za visiwa vya Ryukyu.

Kijapani kinafanana kiasi na Kikorea na kwa kawaida nyingi kimepangwa katika jamii ya lugha za Kialtai. Lakini kuna tabia kadhaa katika Japani ya kale zisizolingana na Kialtai, hivyo majadiliano ya kitaalamu yaendelea.

Lugha imepokea maneno mengi kutoka Kichina.

Mwandiko hariri

Kuna namna tatu ya kuandika:

  • hiragana (ひらがな) ni mwandiko wa kawaida. Alama zake zinaonyesha silabi. Watoto wote wanaanza kujifunza kuandika na kusoma kwa hiragana.
 
Silabi "MU" kwa katakana
  • katakana (カタカナ) ni mwandiko wa silabi pia lakini inatumiwa wa njia maalumu. Kama neno linatakiwa kuangaliwa hasa inaoanyeshwa kwa kutumia alama za katakana (kama maandishi manene au ya kiitaliki). Vilevile hutumiwa kwa maneno yasiyo kawaida kama maneno ya kisayansi au maneno ya kigeni.
  • kanji (漢字) ni alama za asili ya kichina na kila alama ni neno zima si silabi tu. Kijapanai inatumia alama 2,000 za aina hii.

Inawezekana kuandika Kijapani kwa njia mbili:

a) kama Kiswahili cha kisasa kuanzia upande wa kushoto kwenda kulia

b) Kuanzia juu kwenda chini kwa kutumia nhuzo.

Mifano hariri

Inayofuata ni mifano ya maneno ya Kijapani:

  • こんにちは (konnichiwa) : Habari zako! (wakati wa mchana)
  • さようなら (sayōnara) : kwa heri
  • はい (hai) : ndiyo
  • いいえ (īe) : hapana
  • キリスト教 (Kirisuto-kyō) : Ukristo
  • イスラム教 (Isuramu-kyō), イスラーム教(Isurāmu-kyō) : Uislamu
  • 仏教 (Bu-kkyō) : Ubuddha
  • 神道 (Shintō) : Shinto
  • ヒンドゥー教 (Hindwū-kyō), ヒンズー教 (Hinzū-kyō) : Uhindu
  • 平和 (hēwa) : amani
  • 戦争 (sensō) : vita
  • ヨーロッパ (欧羅巴) (Yōroppa), 欧州 (Ōshū) : Ulaya
  • アジア (亜細亜) (Ajia) : Asia
  • アメリカ州 (Amerika-shū) : Amerika
  • オセアニア (Oseania), 大洋州(Taiyō-shū) : Australia na Pasifiki
  • 南極 (Nankyoku), 南極大陸 (Nankyoku tairiku) : Bara la Antaktiki
  • 日本 (Nihon au Nippon), 日本国 (Nihon koku au Nippon koku) : Ujapani, Japani
  • アメリカ(亜米利加) (Amerika), 米国 (Bē-koku), アメリカ合衆国 (Amerika gasshūkoku) : Marekani, Muungano wa Madola ya Amerika
  • 中国 (Chuugoku), 中華人民共和国 (Chūka jinmin kyōwakoku) : Jamhuri ya Watu wa China
  • フランス(仏蘭西) (Furansu), 仏国 (Futsu-koku), フランス共和国 (Furansu kyōwakoku) : Jamhuri ya Kifaransa
  • イギリス(英吉利) (Igirisu), 英国 (Ē-koku), グレートブリテンおよび北アイルランド連合王国 (Gurēto Buriten oyobi Kita Airurando rengō ōkoku) : Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini
  • ロシア(露西亜) (Roshia), ロシヤ (Roshiya), ロシア連邦 (Rosia renpō) : Shirikisho la Urusi
  • アルゼンチン(亜爾然丁) (Aruzenchin), アルゼンチン共和国 (Aruzenchin-kyōwakoku) : Jamhuri ya Argentina
  • オーストラリア(濠太剌利) (Ōsutoraria), オーストラリヤ (Ōsutorariya), オーストラリア連邦(Ōsutoraria renpō) : Jumuiya ya Australia
  • ブラジル(伯剌西爾) (Burajiru), ブラジル連邦共和国 (Burajiru renpō kyōwakoku) : Shirikisho la Jamhuri ya Brazil
  • カナダ(加奈陀) (Kanada) : Kanada
  • ドイツ(独逸) (Doitsu), ドイツ連邦共和国 (Doitsu renpō kyōwakoku) : Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani
  • インド(印度) (Indo) : Jamhuri ya Uhindi
  • インドネシア(印度尼西亜) (Indoneshia), インドネシヤ (Indoneshiya), インドネシア共和国 (Indoneshia kyōwakoku) : Jamhuri ya Indonesia
  • イタリア (伊太利亜) (Itaria), イタリヤ (Itariya), イタリア共和国 (Itaria kyōwakoku) : Jamhuri ya Italia
  • メキシコ(墨西哥) (Mekishiko), メキシコ合衆国 (Mekishiko gasshūkoku) : Maungano a Madola ya Mexiko
  • サウジアラビア (Sauji arabia), サウジアラビア王国 (Sauji arabia ōkoku) : Ufalme wa Uarabuni wa Saudia
  • 南アフリカ共和国(南阿弗利加共和国) (Minami Afurika kyōwakoku) : Jamhuri ya Afrika Kusini
  • 韓国 (Kan-koku), 大韓民国 (Dai Kan minkoku) : Jamhuri ya Korea
  • トルコ(土耳古) (Toruko), トルコ共和国 (Toruko kyōwakoku) : Jamhuri ya Uturuki

Viungo vya nje hariri