Grace Mapunda
Grace Mapunda (maarufu kama Mama Kawele au Tessa; 1969 - 2024) alikuwa mwigizaji wa filamu za Tanzania (Swahiliwood), anayesifika kwa uwezo wake mkubwa wa kuigiza filamu za hisia kutokana na kuwa makini katika kuwakilisha uhusika halisi japo anaonekana kuzipatia filamu za aina hiyo.[1]
Grace Mapunda | |
Amezaliwa | Julai 5, 1969 Mwanza, Tanzania |
---|---|
Amekufa | Novemba 2, 2024 Mwananyamala Referral Hospital, Dar es Salaam |
Nchi | Tanzania |
Majina mengine | Grace Mapunda |
Kazi yake | mwigizaji wa filamu za kitanzania |
Watoto | 2. Happiness and Ritha |
Familia
haririGrace Mapunda amebarikiwa kuwa na watoto wawili (Happiness pamoja na Ritha) ambao baba yao alifariki siku za nyuma. Happiness huigiza na kuimba, aliwahi kuigiza na mama yake katika filamu ya Fake Smile. Ritha naye ni mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya.[1]
Kazi
haririFilamu alizoigiza ni pamoja na House of death, Hard Price, Nilindiwe, Kichupa, Majuto, Mwaka wa Hasara, chloroquine love, Chungu ya Nafsi, Poor Minds, Jibu la ndoto, Back to life na zingine nyingi[1] Batuli.
Maradhi na Kifo
haririGrace Mapunda alipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Msemaji wa familia Aziz Mohamedi aabaye ndiye mzalishaji wa tamthilia pendwa ya Huba ililieleza gazeti la Mwananchi, Grace alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya nimonia mpaka mauti ilipomkuta.[2]
Tanbihi
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-10-31. Iliwekwa mnamo 2018-11-17.
- ↑ "Kilichomuua Grace Mapunda 'Tesa' hiki hapa". Mwananchi (kwa Kiingereza). 2024-11-03. Iliwekwa mnamo 2024-11-04.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Grace Mapunda kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |