Dar es Salaam
Dar es Salaam ni jiji kubwa kuliko yote nchini Tanzania. Pia ni jina la mkoa wake. Dar es Salaam ni mji mkongwe na wenye watu wengi zaidi katika Jumuia ya Afrika Mashariki. Katika Tanzania ndio mji wenye vitega uchumi vingi na ndio mji unaoangaliwa na watu wengi.
- Kwa maana nyingine, tazama Mkoa wa Dar es Salaam
Dar es Salaam | |||
|
|||
Lokeshen Dar es Salaam | |||
Majiranukta: 6°48′0″S 39°17′0″E / 6.8°S 39.28333°E | |||
Nchi | Tanzania | ||
---|---|---|---|
Mkoa | Dar es Salaam | ||
Idadi ya wakazi (2012) | |||
- | 4,364,541 |
Ni mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania wakati Dodoma ni mji mkuu wa Tanzania (kinadharia tangu mwaka 1973). Mpango wa kuhamishia serikali mjini Dodoma unaendelea kwa kasi chini ya rais John Magufuli, japokuwa bado ofisi kadhaa za serikali, ikiwa ni pamoja na Ikulu, zipo Dar es Salaam.
Mji una wakazi wapatao 4,364,541 kwa hesabu ya sensa iliyofanyika katika mwaka wa 2012.[1]
HistoriaEdit
Jiji hili zamani lilikuwa kijiji na kuitwa Mzizima. Sultani Seyyid Majid wa Zanzibar ndiye aliyechagua jina "Dar es Salaam" linalotokana na lugha ya Kiarabu دار السلام (Dār as-Salām) lenye kumaanisha "nyumba ya amani." Maelezo yanayopatikana mara nyingi kuwa maana ni "bandari ya salama" yachanganya maneno mawili ambayo kimatamshi yanafanana kidogo katika lugha ya Kiarabu yaani "dar" (دار = nyumba, makazi) na "bandar" (بندر = bandari). Hadi leo kuna majengo mawili yaliyobaki ya vyanzo hivi ambayo ni Boma la Kale na Nyumba ya Atiman House.
Dar es Salaam ilichaguliwa na wakoloni Wajerumani kuwa mji mkuu wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kwa sababu ya bandari asilia yenye mdomo mpana wa mto Kurasini. Hivyo kuanzia mwaka 1891 Dar es Salaam ilichukua nafasi ya Bagamoyo kama makao makuu ya utawala.
Bandari pamoja na ujenzi wa reli ya kati kwenda Kigoma tangu mwaka 1904 viliimarisha nafasi ya mji ulioendelea kama mji mkuu baada ya Tanzania bara ya leo kuwa eneo lindwa la Tanganyika chini ya Uingereza.
Wakazi na uchumiEdit
Dar es Salaam inakadiriwa kuwa na wakazi wapatao milioni tatu. Ingawa Dodoma inafahamika kama ndio mji mkuu wa Tanzania, Dar es Salaam ndiko ziliko ikulu, mabalozi, mashirika ya kimataifa, n.k.
Uwanja wa ndege mkuu wa Tanzania uko pia mjini hii ni Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.
Bandari ya Dar es Salaam katika bahari ya Hindi, ndio bandari kubwa nchini Tanzania inayojihusisha na usafirishaji na uingizaji wa bidhaa mbalimbali za kilimo, ufugaji, ujenzi, magari, madawa, n.k.
Kiutawala, Dar es Salaam imegawanywa katika manisipaa za Temeke, Ilala, Kinondoni, Kigamboni na Ubungo.
Wakazi na uchumiEdit
Dar es Salaam ni mji unaosemekana kuwa mkubwa kuliko yote kwa sababu ya maendeleo mbalimbali ya viwanda, uwepo wa bahari, uwepo wa sehemu mbalimbali za kihistoria n.k.
Huduma za jijiEdit
Huduma ya maji Dar es Salaam imekuwa na tatizo kubwa katika kudhibiti mfumo wa maji taka katika mkoa wa Dar es Salaam kwa muda mrefu. Tangu shirika la maji DAWASCO (Dar es Salaam Water Supply Company) lilipowekwa rasmi kama shirika husika katika kuratibu utaratibu mzima wa mfumo wa maji safi na maji taka, kumekuwa na nafuu kidogo tu, lakini baada ya muda, liliibuka tatizo la kuibiwa kwa mabomba na uharibifu wa vyanzo mbalimbali vya maji.
ElimuEdit
Kwenye suala hili la elimu vijana wanatakiwa kupewa elimu; hasa vijana wa mitaani wasioingiza kipato inabidi wapewe elimu kwa kazi fulani ili waweze kuajiriwa na kulipa faida taifa kwa kuingizia kipato na kukuza uchumi wa taifa. Mfano wa kazi hizo ni kama ujenzi wa nyumba n.k.
PichaEdit
MarejeoEdit
- ↑ Ripoti ya Sensa 2012. Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-04-24. Iliwekwa mnamo 2013-11-22.
Viungo vya njeEdit
- (Kiingereza) DAR ES SALAAM CITY PROFILE Archived Mei 18, 2006 at the Wayback Machine.
- Mohamed Said: Mwalimu in 1950s Dar (East African October 12 2008 - inasimulia maisha ya Nyerere Dar es Salaam pamoja na habari nyingi za jiji wakati wa miaka ya 1950) Archived Machi 15, 2011 at the Wayback Machine.
- Dar es Salaam kwenye Wikipedia commons